Shinyanga: Kijana mmoja akamatwa na Polisi kwa kumdanganya Waziri Ummy kuwa anaumwa COVID-19

Shinyanga: Kijana mmoja akamatwa na Polisi kwa kumdanganya Waziri Ummy kuwa anaumwa COVID-19

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mussa Jackson Kisinza, (25) mkazi wa kijiji cha Mwakitolyo namba 02 wilaya ya Shinyanga kwa kutoa taarifa ya uongo kwa kumpigia simu na kumdanganya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuwa ana ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba baada ya kijana huyo kutoa taarifa kuwa ana ugonjwa wa Corona timu ya madaktari inayotoa huduma eneo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (vijijini) kuhusiana na ugonjwa wa Covid 19 ilifika eneo la kijiji cha Mwakitolyo namba 02 ili kutoa huduma kwa mtu huyo lakini mtu huyo alizima simu yake na kusababisha timu hiyo ya madaktari kushindwa kumpata hivyo kusababisha taharuki.

“Hivyo Aprili 15,2020 majira ya saa moja kamili asubuhi kikosi kazi cha askari wa makosa ya kimtandao walifika eneo la Mwakitolyo namba 02 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Mussa Jackson akiwa anaendelea na shughuli zake za machimbo na kumfikisha zahanati ya kijiji cha mwakitolyo namba 02”,ameeleza Kamanda Magiligimba.

“Timu ya madaktari ilimfanyia vipimo vya awali vya magonjwa nyemelezi yanayoashiria kuwepo kwa uwezekano wa mtu kuwa na ugonjwa wa Covid 19 lakini hakuwa na dalili za magonjwa hayo”,ameongeza Kamanda Magiligimba.

Amesema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa amekiri kutoa taarifa hiyo na kwamba baadaye aliamua kuiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja.

“Natoa wito kwa wananchi kuacha masihara juu ya ugonjwa Covid 19 na mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo juu ugonjwa huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema.
 
Kadanganya kwani ana vipimo ?
Yeye kwa upeo wake amedhani anayo, sasa kama hana si bahati nzuri ?
Tunatumia nguvu nyingi kwa vitu ambavyo tungeweza kuvipuuza..., sasa na mimi kesho nikidhani ninayo si taogopa kupiga simu nisihukumiwe kudanganya ?
 
Sasa kamdanganya vipi ikiwa anaona na kuhisi dalili ambazo aliziona kwenye Luninga Au Redioni kuwa ukiona dalili zifuatazo wahi kituo cha Afya au piga 911?
 
Duuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu unadhani huyo mtuhumiwa baada ya kupiga simu na kudai kua ana maambukizi ya Corona ni kwanini aliiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja? umejiuliza hilo swali?
 
Kadanganya kwani ana vipimo ?
Yeye kwa upeo wake amedhani anayo, sasa kama hana si bahati nzuri ?
Tunatumia nguvu nyingi kwa vitu ambavyo tungeweza kuvipuuza..., sasa na mimi kesho nikidhani ninayo si taogopa kupiga simu nisihukumiwe kudanganya ?
Sasa kamdanganya vipi ikiwa anaona na kuhisi dalili ambazo aliziona kwenye Luninga Au Redioni kuwa ukiona dalili zifuatazo wahi kituo cha Afya au piga 911?
Wakati mwingine muwe mnasoma content! Kama ni dalili alikuwa nazo kwanini azime simu na kuvunjavunja line? Na hakuna sehemu amesema alikuwa anajisikia dalili moja mbili tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mwingine muwe mnasoma content! Kama ni dalili alikuwa nazo kwanini azime simu na kuvunjavunja line? Na hakuna sehemu amesema alikuwa anajisikia dalili moja mbili tatu

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa kati yangu mimi na wewe sijui nani sio makini..., hii habari imekuwa edited mwanzoni ililetwa nusu kwa maandishi kwamba habari zaidi zitaendelea..., au wewe mgeni humu hujui kuna editing after the fact...
 
Sent using Jamii Forums mobile app
[/QUOTE]
Kadanganya kwani ana vipimo ?
Yeye kwa upeo wake amedhani anayo, sasa kama hana si bahati nzuri ?
Tunatumia nguvu nyingi kwa vitu ambavyo tungeweza kuvipuuza..., sasa na mimi kesho nikidhani ninayo si taogopa kupiga simu nisihukumiwe kudanganya ?
Sasa kamdanganya vipi ikiwa anaona na kuhisi dalili ambazo aliziona kwenye Luninga Au Redioni kuwa ukiona dalili zifuatazo wahi kituo cha Afya au piga 911?
Duuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili

Sent using Jamii Forums mobile app
Someni muelewe, huyu jamaa baada ya kutoa taarifa akavunja laini na timu ya madaktari ilipofika kumpa huduma wakamkosa. Hii inamaana alikuwa anajua alitendalo kwamba anadanganya. Angeruhusu madaktari wampe huduma halafu asikutwe na covid 19, hapo isingekuwa kosa
 
Wasukuma wana nini jamani??😀😀
Akaamua kutupa line aliyosajili kwa NIDA?

Everyday is Saturday......................😎
 
Back
Top Bottom