Makuku Rey
JF-Expert Member
- Dec 31, 2013
- 3,497
- 3,823
Nilihisi kupona kabisa baada ya kujifukiza moshi wa mavi ya tembo, ko nikaona wasihangaike kuja kunichukua wakati nahisi kupona mafua.Mkuu unadhani huyo mtuhumiwa baada ya kupiga simu na kudai kua ana maambukizi ya Corona ni kwanini aliiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja? umejiuliza hilo swali?
Kama alikuwa mgonjwa kwanini alizima simu yake na.kuendelea na shuhuli zake, mgonjwa angeenda kazini na kuendelea shuhuli zake? Siku akiumwa kweli atakosa wakimsaidia watajua ni utaniDuuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
Sio kosa. Piga simu, eleza uko wapi, wahusika watakuja na kukufanyia vipimo. Huna wanakueleza kiungwana kabisa. Kosa, umepiga simu, wahusika wamekuja umejificha na kuzima simu yako. Hebu angalia usumbufu huo! Tujaribu kutafakari kwanza kabla ya kukimbilia kulaumu.Duuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili
Sent using Jamii Forums mobile app
uli HISI..!!! Ugonjwa haujulikani kwa hisia bali kwa vipimo na kuthibitishwa scientifically.Nilihisi kupona kabisa baada ya kujifukiza moshi wa mavi ya tembo, ko nikaona wasihangaike kuja kunichukua wakati nahisi kupona mafua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa haikuwa imekamilika mwanzo sisi sio wajinga hadi tu-komenti vileSent using Jamii Forums mobile app
Someni muelewe, huyu jamaa baada ya kutoa taarifa akavunja laini na timu ya madaktari ilipofika kumpa huduma wakamkosa. Hii inamaana alikuwa anajua alitendalo kwamba anadanganya. Angeruhusu madaktari wampe huduma halafu asikutwe na covid 19, hapo isingekuwa kosa
Nilijua tu atakuwa migodini..wakitokaga migodini ile jioni utawaona na visimu vyao sasa...hahha kukosa kazi huko!Wasukuma bwana!
Tayari Corona kwao ujiko! 😁😃😅😆😂😂🤣
Ndo wamekuja wamenipima scientifically wamesema sina dalili zozote na siumwi, ko nilimdanganya waziri Kumbe mi nshapona kwa mavi ya tembo.uli HISI..!!! Ugonjwa haujulikani kwa hisia bali kwa vipimo na kuthibitishwa scientifically.
Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mussa Jackson Kisinza, (25) mkazi wa kijiji cha Mwakitolyo namba 02 wilaya ya Shinyanga kwa kutoa taarifa ya uongo kwa kumpigia simu na kumdanganya Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuwa ana ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba baada ya kijana huyo kutoa taarifa kuwa ana ugonjwa wa Corona timu ya madaktari inayotoa huduma eneo la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (vijijini) kuhusiana na ugonjwa wa Covid 19 ilifika eneo la kijiji cha Mwakitolyo namba 02 ili kutoa huduma kwa mtu huyo lakini mtu huyo alizima simu yake na kusababisha timu hiyo ya madaktari kushindwa kumpata hivyo kusababisha taharuki.
“Hivyo Aprili 15,2020 majira ya saa moja kamili asubuhi kikosi kazi cha askari wa makosa ya kimtandao walifika eneo la Mwakitolyo namba 02 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Mussa Jackson akiwa anaendelea na shughuli zake za machimbo na kumfikisha zahanati ya kijiji cha mwakitolyo namba 02”,ameeleza Kamanda Magiligimba.
“Timu ya madaktari ilimfanyia vipimo vya awali vya magonjwa nyemelezi yanayoashiria kuwepo kwa uwezekano wa mtu kuwa na ugonjwa wa Covid 19 lakini hakuwa na dalili za magonjwa hayo”,ameongeza Kamanda Magiligimba.
Amesema baada ya kuhojiwa mtuhumiwa amekiri kutoa taarifa hiyo na kwamba baadaye aliamua kuiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja.
“Natoa wito kwa wananchi kuacha masihara juu ya ugonjwa Covid 19 na mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo juu ugonjwa huo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake”,amesema.
Mawazo yako yanaendani kabisa na Avatar uliyoweka.Ndo wamekuja wamenipima scientifically wamesema sina dalili zozote na siumwi, ko nilimdanganya waziri Kumbe mi nshapona kwa mavi ya tembo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kadanganya kwani ana vipimo ?
Yeye kwa upeo wake amedhani anayo, sasa kama hana si bahati nzuri ?
Tunatumia nguvu nyingi kwa vitu ambavyo tungeweza kuvipuuza..., sasa na mimi kesho nikidhani ninayo si taogopa kupiga simu nisihukumiwe kudanganya ?
Duuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili
Sent using Jamii Forums mobile app
Shida ya hii nchi kila mtu anajifanya mjuaji. Yaani wanaleta utoto hadi kwenye vitu vya msingi. Ameshasahau kwamba huyo mtu ameivunja lain lakini pia mtuhumiwa akili ni ndogo lain ameisajili anafikiri kuvunja lain ndiyo kufuta jina lake. Yaani huku nyuma ya keyboard ni shida kweli.Mkuu unadhani huyo mtuhumiwa baada ya kupiga simu na kudai kua ana maambukizi ya Corona ni kwanini aliiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja vunja? umejiuliza hilo swali?
Duuu we jamaa umefikiriaje kumwita naman hiyo....kakuzingua sana eti...
Mawazo yako yanaendani kabisa na Avatar uliyoweka.
Mbona mtuhumiwa alizima simu yake na kuvunja vunja SIM card ili kuharibu ushahidi hata kabla ya vipimo? Na kwa nini ampigie ummy kama si kujitakia ujiko wa kuandikwa Kwenye vyombo vya habari.Duuuh kwa mfano ukijihisi Una covid19 na ukatoa taarifa sehemu husika na wakakupima ukakutwa huna covid19 inakua ni kosa kisheria , aisee hii Nchi kazi tunayo aisee , kwa afadhali watu wakae kimya Kama anajihis
Mungu tunusuru tu na janga hili
Sent using Jamii Forums mobile app
Na kama hana vipimo alijuaje ana corona mpaka kufikia hatua ya kupiga simu kwa waziri halafu baadae akaivunja vunja line ya simu?Kadanganya kwani ana vipimo ?
Yeye kwa upeo wake amedhani anayo, sasa kama hana si bahati nzuri ?
Tunatumia nguvu nyingi kwa vitu ambavyo tungeweza kuvipuuza..., sasa na mimi kesho nikidhani ninayo si taogopa kupiga simu nisihukumiwe kudanganya ?