Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Maafisa wa Maendeleo ya Jamii katika halmashauri za Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuacha urasimu katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha wananchi kunufaika kwa wakati.
Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Shinyanga, Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Christina Mnzava, ameeleza kuwa wananchi wanaopaswa kunufaika na mikopo hiyo wamekuwa wakizungushwa kwa zaidi ya mwezi bila mafanikio.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Wananchi wanazungushwa sana wanapofuatilia mikopo hii. Maafisa wa maendeleo ya jamii wamekuwa wakisumbua wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo, hali inayokifanya Chama cha Mapinduzi kuonekana hakijali wananchi wake," amesema Dkt. Mzava.