Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, wamepokea, kujadili na kupitisha pendekezo la kugawa Jimbo la Solwa, kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Solwa na Itwangi.
Wamepitisha pendekezo hilo jana, Machi 11, 2025 kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani, kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya pendekezo la kugawa Jimbo la Solwa kwamba kuwe na majimbo mawili ya uchaguzi, Solwa na Itwangi,
Awali Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Oscar Lupavila, akiwasilisha taarifa kwa Madiwani kwa niaba ya Mkurugenzi, amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, ilitangaza kuligawa Jimbo la Solwa na kutoa vigezo vyake 10, pia madiwani wanapaswa kujadili na kupitisha mapendekezo ya kuligawa jimbo hili.
Amesema Jimbo la Solwa, kwa sasa linakadiriwa kuwa na watu 503,167 kufikia 2025, kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, jimbo hilo lilikuwa na watu 468,611.
Amesema Jimbo la Solwa likigawanywa, litakuwa na Watu 309,821 na Itwangi 193,346 na kwamba kati ya vijiji 126 na vitongoji 856, kuwa Solwa itakuwa na vijiji 68 na vitongoji 478,huku Itwangi itakuwa na vijiji 58 na vitongoji 378.
“Jimbo la Solwa kwa sasa lina ukubwa wa Kilomita za Mraba 4,212, likigawanywa, Solwa itabaki kuwa na kilomita za mraba 2,573.29, na Jimbo la Itwangi, litakuwa na Kilomita za Mraba 1,638.71,”amesema Oscar.
Ameendelea kueleza kuwa, Jimbo la Solwa litakuwa na Tarafa ya Nindo pamoja na Kata 12; Itwangi itakuwa na Tarafa mbili ya Itwangi na Samuye na kwamba Samuye ina Kata 4; Itwangi Kata 10 jumla zitakuwa Kata 14.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Nicodemus Simon aliandika:
"Vigezo vyote ambavyo vimetolewa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kuligawa Jimbo hili la Solwa tumekidhi, tuombe Mungu ligawanywe na nitafurahi kuona Madiwani mkijitokeza kugombea Ubunge katika Jimbo hili jipya la Itwangi sababu nyie ndiyo mnajua zaidi changamoto za wananchi,”
Source: Nipashe