Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
WanaJF,
Mada hii itakuwa na 'Updates' za Matukio kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani 2025 kama yanavyotujia kutoka kwenu kutoka mkoa wa Shinyanga. Ukiwa na taarifa yoyote ambayo ni ya eneo hili tafadhali usisite kuweka.Mkoa wa Shinyanga uko Kanda ya Ziwa katika Tanzania na ni maarufu kwa shughuli za kilimo na ufugaji, pamoja na madini, hasa almasi. Mkoa huu una historia ya utajiri wa madini, hususan kupitia mgodi maarufu wa almasi wa Mwadui.
Idadi ya Watu
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Shinyanga ni 2,241,299; wanaume 1,102,879 na wanawake 1,138,420, na ina wilaya 5 ambazo ni Shinyanga Manispaa, Shinyanga Vijijini, Kahama Mjini, Kahama Vijijini, UshetuIdadi ya Majimbo ya Uchaguzi
Mkoa wa Shinyanga una jumla ya majimbo 6 ya uchaguzi:- Jimbo la Shinyanga Mjini
- Jimbo la Solwa
- Jimbo la Kahama Mjini
- Jimbo la Msalala
- Jimbo la Kishapu
- Jimbo la Ushetu
Mkoa wa Shinyanga ulishiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliibuka na ushindi mkubwa katika maeneo mengi ya mkoa huo.
Mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM, Hayati John Pombe Magufuli, alipata kura nyingi zaidi kulinganisha na wapinzani wake.
Katika uchaguzi wa Ubunge, wagombea wengi wa CCM walipita bila kupingwa na wengine kushinda kwa kura nyingi dhidi ya wapinzani wao huku wakiwa na ushindi wa 100%.
Uchaguzi wa Madiwani, (CCM) walipata ushindi mkubwa kwenye nafasi za madiwani ikifanikiwa kushinda kata nyingi. Hii ilitokana na upinzani kukumbwa na changamoto nyingi, zikiwemo wagombea wao kuenguliwa kutokana na matatizo ya kisheria au kutokidhi vigezo
Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa vyama vya upinzani kama vile CHADEMA na ACT-Wazalendo kuhusu kutokuwepo kwa uwazi na haki katika mchakato wa uchaguzi.
Updates
December, 2024
- Kuelekea 2025 Ntobi aomba radhi kwa kauli zake kuhusu Tundu Lissu
- Kuelekea 2025 Emmanuel Ntobi: Nimeonewa kwa sababu namuunga mkono Mbowe kwenye Uchaguzi wa chama chetu
February
- Pre GE2025 - Video: Innocent Bashungwa naye atinga mtaani kula kwenye mgahawa pamoja na wananchi. Tunamshukuru Rais Samia!
- Pre GE2025 - Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM- Mhandisi James Jumbe, ajinasibu kuwa CCM itashinda 2025
- Pre GE2025 - Bananga (Katibu wa siasa na uenezi CCM, DSM) asema No reform No election ni kauli ya kiwendawazimu
- Pre GE2025 - Wananchi kutoka Vijiji 112 kutoka Ushetu, Shinyanga wanatarajia kuanza kunufaika na Mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria, mabomba lukuki yashushwa
- Pre GE2025 - Mbunge wa Shinyanga Mjini Patrobas Katambi amuombea kura za Urais Rais Samia kuelekea Uchaguzi Mkuu. CCM mmeanza kampeni?
- Pre GE2025 - Medard Kalemani: CCM Chato tunahita utulivu na umoja kwenye kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi
- Pre GE2025 - Shinyanga: Maafisa mikopo watajwa kusababisha CCM kuchukiwa na wafanyabiashara