Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Polisi Mkoa wa Shinyanga limefukua mwili wa Asha Mayenga (62), mkazi wa Lugela, Kata ya Nyamhanga, Manispaa ya Kahama uliofukiwa shambani, baada ya kutoweka kwa siku tano.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa, Januari 17, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi, amesema mwili huo umekutwa ukiwa umefukiwa jirani na shamba lake la mpunga, lililopo Kijiji cha Malindi, Kata ya Busoka, wilayani humo.
Amesema taarifa za uchunguzi wa awali zinaonyesha mama huyo alikuwa na mgogoro wa shamba na mtoto wake wa kiume.
Soma Pia: Kilimanjaro: Mwanamke mmoja Amuua mama yake mzazi ili arithi shamba
Kamanda amesema Polisi linamshikilia mtoto wa marehemu na wenzake wawili kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
Naye, Mayenga Ng'ombe, mtoto wa marehemu Asha, amedai baada ya ndugu yake (mtuhumiwa) kurejea na kuanza kuhamisha vyombo kwa madai kuwa anahama na kwenda kujitegemea alihisi kuna jambo lisilo la kawaida.