SHINYANGA MJINI: Mkutano Mkuu Jimbo la Shinyanga Mjini wamkataa Mbowe Uenyekiti wasema siasa za sasa zinamkataa Mbowe na kumkubali Lissu

Newforce

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2024
Posts
430
Reaction score
708

View: https://youtu.be/nLcsl_rWxOo?si=WdH5BrwfPwM-IdSl
===
Wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) @ChademaTz kutoka Jimbo la Shinyanga Mjini wametoa msimamo wao kuhusu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Januari 21, 2025.

Katika mkutano maalum uliofanyika jimboni humo, wajumbe wa ngazi mbalimbali wameeleza maoni yao waziwazi, wakimpendekeza Tundu Lissu @TunduALissu kuchukua nafasi hiyo badala ya Mwenyekiti wa sasa, Freeman Mbowe @freemanmbowetz .

Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, Hamisi Ngunila, amesema kuwa maoni ya wanachama ni ya msingi, na viongozi wanapaswa kuyaheshimu kwa kuwa ndio msingi wa ujenzi wa chama.

“Wanachama hawa ndio wanaolipia ada, wanakijenga chama, na wameonyesha wazi kwamba wanamuhitaji Tundu Lissu kwa wakati huu. Mbowe ameongoza kwa muda mrefu na mbinu zimeisha. Tunahitaji kiongozi mpya mwenye nguvu ya kupambana na siasa za CCM na kuleta mabadiliko tunayohitaji,” amesema Ngunila.

Aidha, amebainisha kuwa maoni ya wanachama yametolewa kwa uwazi, si kwa misingi ya ukabila, bali kutokana na rekodi ya Lissu kama mpambanaji wa haki za kidemokrasia, ikiwemo azma yake ya kupata Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya.

Katibu wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini, Sebastian Polepole, ameunga mkono pendekezo hilo, akimshukuru Mbowe kwa mchango wake katika chama lakini akisisitiza kuwa ni wakati wa kupisha kizazi kipya cha uongozi.

“Mbowe kama mchungaji, kwa umri wake wa miaka 68, afungue kanisa. Tumempa nafasi lakini kuna maeneo ameonyesha mapungufu, hususan kuwasaidia wagombea wetu waliojitolea kwa rasilimali zao katika chaguzi kadhaa. Tundu Lissu ana uwezo wa kuleta nguvu mpya na kuimarisha chama,” amesema Polepole.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini (BAZECHA), Bushiri Juma, amesisitiza kuwa wanachama wamechoshwa na hali ya sasa na wanahitaji mabadiliko ya uongozi.

“Wanachama wametutuma tukamlete Tundu Lissu. Wamesema iwapo haitafanyika, wako tayari kuacha shughuli za chama. Mbowe abakie kama mzee wa busara ndani ya chama, lakini nafasi ya uongozi aachie wengine,” amesema Bushiri.

Viongozi wa jimbo hilo wametoa wito kwa viongozi wa majimbo mengine nchini kutumia utaratibu wa kusikiliza maoni ya wanachama wao kuhusu uongozi wa taifa.

Kwasababu maoni ya wanachama ni maoni ambayo ndiyo yanakijenga chama chetu ili tuweze kutengeneza mtandao mpana huku chini lazima tuheshimu maoni yao, ninawashauri hata wenyeviti wa majimbo mengine watumie utaratibu huu kupokea maoni na mawazo ya wanachama ngazi za chini juu ya uchaguzi wa kitaifa wa CHADEMA", amesema Ngunila.

===
 
Mbowe asiwe kama Kenge, mpaka aone damu ndio ajue kuwa ameumia
 
Siasa za hovyo kabisa. Sanduku la kura lipo na ndio mwamuzi.

Halafu wanajiita chama cha demokrasia!
 
Balaa na nusu
 
Back
Top Bottom