LGE2024 Shinyanga: TAKUKURU yathibitisha uwepo wa rushwa kwenye Uchaguzi. Yadokeza Machawa kupelekwa Mbuga Za Wanyama na wapinzani kuhongwa ili wajitoe

LGE2024 Shinyanga: TAKUKURU yathibitisha uwepo wa rushwa kwenye Uchaguzi. Yadokeza Machawa kupelekwa Mbuga Za Wanyama na wapinzani kuhongwa ili wajitoe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, hivi karibuni imeficchua kwamba baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanatoa rushwa kwa wagombea ili kujitoa kwenye uchaguzi na hivyo kuwapa nafasi wagombea wao kupita bila upinzani.

Soma pia: Sarakasi za Chaguzi za Serikali za Mitaa: Je, Nani Alaumiwe?

Akiongea na waandishi wa habari tarehe 11 Novemba 2024, Mkuu wa TAKUKURU Kahama, Abdallah Urari, amesema kuwa uchunguzi umeonesha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanajaribu kuwashawishi wagombea kwa kuwapa rushwa ili wasirudishe fomu au wazijaze kwa makosa, jambo linalopelekea kuenguliwa kwao.

Urari amesisitiza kuwa tabia hii ni kinyume na maadili ya uchaguzi na inalenga kuharibu utaratibu wa uchaguzi.

TAKUKURU imeahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale watakaopatikana na hatia ya kuhusika na vitendo hivi.

Aidha, Urari ameeleza kwamba baadhi ya viongozi wanaunda vikundi maalum vya vijana wanaoitwa "machawa," ambao hutumika kugawa rushwa wakati wa uchaguzi.

Vijana hao wamekuwa wakipewa ahadi za nafasi za uongozi endapo wagombea wao watashinda.

Mbali na hayo, vijana hawa wamekuwa wakipata zawadi na kufadhiliwa kufanya sherehe, ikiwa ni pamoja na kupelekwa kwenye mbuga za wanyama.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom