Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Naona sasa mwaka wa Uchaguzi umewadia na mambo yamekuwa mengi kweli kweli.
Wanasiasa wengine wanaenda kutafuta malisho ya kijana kibichi
===================
Wanachama 18 wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA, Wakiwemo Viongozi wa jumuiya mbalimbali za chama hicho Halmashauri ya Ushetu Mkoani Shinyanga wamekabidhi kadi zao na kuhamia rasmi katika Chama cha Mapinduzi CCM.
Wakizungumza wakati wa kutambulisha katika kikao kazi za Kamati ya Siasa ya kata Kisuke baadhi ya Wanachama hao Emmanuel Machibya na Seleman Ramadha Shija Wamesema kuwa matamanio yao ilikuwa ni kuona Ushetu ikifunguka hasa katika sekta ya usafirishaji na Kazi hiyo imefanyika ipasavyo katika kipindi cha Uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe Emmanuel Cherehani hivyo hawana budi kuwaunga mkono.
Hata hivyo CCM pia imepokea wanachama wengine watano kutoka TLP na mmoja wa NCCR Mageuzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa kata hiyo Mwl. Doto Misungwi amesema ujio wa wanachama hao wapya ndani ya chama chao ni ishara tosha kwamba ilani inatekelezwa kwa uhakika huku Mbunge Cherehani akiwaahidi kuwapa ushirikiano na kuendelea kuwahudumia Wananchi wote kwa usawa bila kujali tofauti za Vyama vyao wala imani zao za dini.