Shinyanga: Watatu wakamatwa kwa kutapeli Watu wakijidai ni Usalama wa Taifa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watuhumiwa watatu Dismond Zakaria ambaye ni Mwalimu (33) Feisal Husein Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano (27) na Juma Almasi (35) Mfanyabiashara kwa tuhuma ya kupatikana na nyaraka za Serikali za kughushi kwa lengo la kufanya utapeli kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Kahama Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mei 26 mwaka huu katika mtaa wa namanga wilayani humo katika msako maalumu wa kupambana na wahalifu.

Amesema kuwa baada ya kukamatwa walipatikana na nyaraka mbalimbali za Serikali ikiwemo Kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, Vitambulisho viwili vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mhuri mmoja na barua mbalimbali zenye nembo ya Jeshi la hilo.

“Watuhumiwa hawa hutumia magari mawili kufanya utapeli katika maeneo mbalimbali ya Tanzania yenye namba za usajili T 677 BMA Toyota Carina na T 110 DSX Toyota Rumion kwa kujiwasilisha kwa wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kuwa wao ni maafisa wa umma na wakifanikisha azima yao hutoroka,” Magilimba.

Kamanda Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wanatumia Vitambulisho vya Jeshi la wananchi viwili vyenye Cheo cha Kanali na kimoja cha Idara ya Usalama wa Taifa, pamoja na sare kwa lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia fedha kwa njia isiyo halali huku wakijua wazi kuwa suala hilo ni kinyume cha sheria.

“Tumewakamata wakiwa na karatasi bandia zinazotumika kutapelia watoa huduma za za fedha,walikuwa wanatumia mbinu ya kuacha mabegi yao yenye karatasi hizo bandia katika ofisi hizo na kisha hurudi jioni na kuwaaminisha kuwa ni fedha halali, jambo ambalo halina ukweli wowote,” Magiligimba.

Amefafanua kuwa mbinu nyingine inayotumiwa na watuhumiwa hao ni pamoja na kuwatongoza na kuwanywesha pombe wanawake na kuwaibia vitu vya thamani kama vile simu na fedha pamoja na kuwaahidi kuwapatia kazi kwa idara ya usalama wa taifa na jeshi la wananchi wa Tanzania.

“Bado tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapowatilia shaka watu wanamna hiyo ambao hutumia vibaya nyaraka za serikali kujipatia kipato kwa njia isiyo halali,” Magiligimba.

Millard Ayo
 
Mbinu ya sabaya na genge lake la wahalifu lipo shinyanga pia kuna wale maofisa feki wa TRA. Walio kamatwaga Tanga wakitembelea gari aina ya Toyota prado namba za gari sizikumbuki.
 
Kuna haja sasa ya kubadili sheria ya uendeshaji wa makosa ya jinai ili ikidhi zama hizi za teknohama.

Lakini pia elimu kwa jamii itolewe maana nguvu inayotumika kwa polisi na Idara nyingine za usalama ni kubwa sana huwezi kuhoji na hiyo hutoa mwanya kwa wahalifu hasa ukizingatia raia wengi hawana uelewa wa kutosha.
 
Polisi ni dhaifu sana, kwanini ikamate watu ambao wameshatapeli kwa muda mrefu hivi wakati wanaanza polisi walikuwa wapi na intelijensia yao?!
Ukiona hivi ujue wamegombana kwenye mgao maana polisi wetu wanahusika kwa kila uhalifu unaotendeka hapa nchini trust me!

Mbaya zaidi IGP anawatetea sana polisi wake kama juzi eti kapiga marufuku mgambo kukaa vituo vya polisi kwa madai wanaomba na kupokea rushwa na kulichafua jeshi lake! Mgambo sio wanaoweka watuhumiwa mahabusu bure na kuwataka watoke kwa laki 3 hadi milioni 3, mgambo sio wanaowapa mahabusu simu wazungumze na ndugu zao ili wamletee pesa ocd na oc cid ili waachiwe, mgambo sio wanaobambika kesi kwa mtu aliyeonekana ana pesa nyingi hivyo wakatamani wamnyang'anye hiyo. IGP sidhani kuwa huyajui haya ila unaogopa kuchukua hatua!
 
Kuwa usalama wa taifa sio lazima ufanye kazi TISS, Police au TPDF. Hata kama haufanyi kazi TISS, Polisi au JWTZ, wewe kama raia mwema bado una jukumu la kuwa mlinzi wa Tanzania ukianzia katika eneo/kijiji unachoishi.

Kama raia mwema unaweza ukashiriki katika usalama wa taifa lako kwa kutoa ushirikiano kuanzia ngazi ya mjumbe, serikali ya mtaa wako au ikiwezekana toa taarifa hata kituo kidogo cha polisi kilicho karibu yako pindi uonapo dalili ama vitendo vya uvunjifu wa amani.

Kuwa mtu wa usalama wa taifa ni pamoja na kukusanya vijana wenzako na kuwapa elimu ya afya (ulevi/mihadarati) na usalama barabarani hivyo kuwafanya kuwa maderava wazuri wa bodaboda watakaoepusha ajali za kizembe na wanaojitambua wasiovuta bangi wala kunywa gongo.

Unakuta kijana anatamani kufanya kazi TISS au kuwa askari Jeshi lakini wanafunzi wa secondary na primary wanapewa mimba na wahuni mtaa anapoishi anashindwa kwenda kutoa taarifa ofisi ya serikali ya mtaa, kwa mjumbe au hata kituo cha police kilicho karibu yake.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watuhumiwa watatu Dismond Zakaria ambaye ni Mwalimu (33) Feisal Husein Mtaalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano (27) na Juma Almasi (35) Mfanyabiashara kwa tuhuma ya kupatikana na nyaraka za Serikali za kughushi kwa lengo la kufanya utapeli kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Wilayani Kahama Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga (ACP) Debora Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa mei 26 mwaka huu katika mtaa wa namanga wilayani humo katika msako maalumu wa kupambana na wahalifu.

Amesema kuwa baada ya kukamatwa walipatikana na nyaraka mbalimbali za Serikali ikiwemo Kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, Vitambulisho viwili vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Mhuri mmoja na barua mbalimbali zenye nembo ya Jeshi la hilo.

“Watuhumiwa hawa hutumia magari mawili kufanya utapeli katika maeneo mbalimbali ya Tanzania yenye namba za usajili T 677 BMA Toyota Carina na T 110 DSX Toyota Rumion kwa kujiwasilisha kwa wafanyabiashara hususani watoa huduma za kifedha kuwa wao ni maafisa wa umma na wakifanikisha azima yao hutoroka,” Magilimba.

Kamanda Magiligimba amesema kuwa watuhumiwa hao wanatumia Vitambulisho vya Jeshi la wananchi viwili vyenye Cheo cha Kanali na kimoja cha Idara ya Usalama wa Taifa, pamoja na sare kwa lengo la kuwahadaa wananchi ili kujipatia fedha kwa njia isiyo halali huku wakijua wazi kuwa suala hilo ni kinyume cha sheria.

“Tumewakamata wakiwa na karatasi bandia zinazotumika kutapelia watoa huduma za za fedha,walikuwa wanatumia mbinu ya kuacha mabegi yao yenye karatasi hizo bandia katika ofisi hizo na kisha hurudi jioni na kuwaaminisha kuwa ni fedha halali, jambo ambalo halina ukweli wowote,” Magiligimba.

Amefafanua kuwa mbinu nyingine inayotumiwa na watuhumiwa hao ni pamoja na kuwatongoza na kuwanywesha pombe wanawake na kuwaibia vitu vya thamani kama vile simu na fedha pamoja na kuwaahidi kuwapatia kazi kwa idara ya usalama wa taifa na jeshi la wananchi wa Tanzania.

“Bado tunaendelea kuwahoji na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa pindi wanapowatilia shaka watu wanamna hiyo ambao hutumia vibaya nyaraka za serikali kujipatia kipato kwa njia isiyo halali,” Magiligimba.

Millard Ayo
Katika watu wanaopenda kujipa mamlaka za serikali ni watu wakutoka kanda hiyo sijui wanashida gani!

Sent from my 601SO using JamiiForums mobile app
 
Oya mmbo vpiii ww ni mwenyeji wa kahama mkuu nahitaji mwenyeji wa kahama kwenye jukwaa hiliii nina vitu nahitaji kujua kuhusu hapo kaham kama hutojal nicheki PM au WhatsApp 0653271318
stoplight
 
Back
Top Bottom