SHIP SCRAPING/SHIP BREAKING

SHIP SCRAPING/SHIP BREAKING

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
SHIP BREAKING/SHIP RECYLING/SHIP DEMOLITION/SHIP CRACKING/SHIP DISMANTLING

Hii ni kitendo cha ukataji wa meli kwa ajili ya kutoa vipuri, malighafi za vyuma ambazo zinaweza zikatumika tena au chuma kuyeyushwa kama chuma chakavu.


Meli nyingi za miaka ya sasa umri wa kuishi ni kuanzia miaka 25 mpaka 30 kabla ya sehemu nyingi kuathiriwa na kutu, vyuma kuporomoka na meli kuwa na gharama kubwa kuihudumia kutokana na uchakavu.

1681127440158.jpeg


MATUMIZI YA CHUMA NA VIFAA BAADA YA MELI KUKATWA

Chuma kutoka melini huyeyushwa tena kwa matumizi mengine, kutengeneza vitu mbalimbali na vyuma kwa ajili ya ujenzi na mitambo.

Vifaa kama Air Conditions, fridges,washing machines,pumps,generators, workshop tools na engines huuzwa na kutumika kama vitu used.

M4JsCuxmeJ4golOcrm5sBJEJvhUJIaIsrqOlMdZvklY.jpg

1681128152643.jpeg
OIP._5bhTWjbE3XJSnJA_KzLxwHaFj


SEHEMU ZA UKATAJI MELI

Hii kazi imekuwa ikifanyika kwenye nchi maskini sababu kubwa ni kuwa inahitaji nguvu kazi kubwa ya watu na pia ni kazi inayohatarisha uchavuzi wa mazingira. Asilimia 92 ya meli mnamo mwaka 2013 zilikatwa katika bara la Asia. Mpaka mwaka 2020 Alang Ship Breaking Yard iliyopo nchini India ilikuwa[M1] imefanya 30% ya ukataji wa meli zote ikifatiwa na Chittagong Ship Breaking Yard iliyopo Bangladesh na Gadani Ship Breaking Yard iliyopo Pakistan.



Bangladesh wanapata 20% ya matumizi ya nchi kwenye chuma kutokana na meli zilizokatwa, India wao wanapata 10% ya chuma kutokana na meli zilizokatwa. Africa nchi ya Namibia na Mauritius shughuli za ukataji meli unafanyika kwa kiasi.



NJIA MBADALA ZA UKATAJI MELI

Njia mbadala za kukata meli ni kuizamisha na kuweka mnara wa tahadhari na kuweka alama kuonyesha uwepo wa meli iliyozama. Meli huzamishwa kwenye Bahari kuu au kina kirefu pia kuna njia ya kuileta kwenye fukwe ambazo hazitumiki na kutumika kama makumbusho au sehemu ya watu kutalii na kujifunza.

OIP.URFLVNjQuMCJ4zqOeinJlAHaEK


UFANYAJI KAZI NCHI ZILIZOENDELEA

Nchi zilizoendelea hufanya kazi hizi kwa kufuata sheria za mazingira ya nchi husika. Meli kabla ya kukatwa hukaguliwa na jopo la wataalamu wa mazingira na kupata tathmini ya kazi. Meli hutolewa oil, mafuta, vilainishi vyote na uchafu wa maji taka. Pia hutumia zana za kisasa katika ukataji vyuma vya meli na mitambo wakati wa kubeba vyuma.



UFANYAJI KAZI NCHI ZINAZOENDELEA

Nchi kama Bangladesh,India na Pakistan zimekuwa sehemu kuu ya ukataji wa meli chakavu duniani. Mwaka 2006 mahakama kuu ya India ilikataa zoezi la kukata meli ya Kijeshi ya Ufaransa kutokana na kuhofia athari za kimazingira. Meli hii ya kijeshi ikaja kukatwa baadae na kampuni ya Uingereza.



Mwaka 2009 Bangladesh Environmental Lawyer Association ilishinda kesi na kutoa amri ya kukataza meli zote zisizo na ubora kutokwenda kukatwa nchini humo. Hali hii ilipelekea miezi 14 shughuli za ukataji meli kusimama nchini humo na maelfu ya wananchi wakakosa kazi. Baadae katazo hilo likatolewa na serikali na ukataji wa meli ukaendelea mpaka sasa.

Asilimia kubwa ya meli zinazokatwa ni zile ambazo zimeezeka na gharama ya kuzihudumia imefika hatua ni kubwa.Nchi maskini hutumia nguvu kazi kuwa ya watu katika kazi hii za ukataji meli.

1681127487520.jpeg


MAUZIANO YA MELI

Madalali wa meli (Shipbrokers) hawa hupewa meli na specification zake kisha huwaunganisha mmiliki na mnunuaji kwa ajili ya makubaliano na wao hulipwa kwa kamisheni kulingana na biashara. Shipbrokers wengi kampuni zao kubwa zipo London,Singapore,Thailand na Hong Kong.



Bei za meli chakavu hukadiriwa kwa tani moja ya kilo ya chuma, ambapo wastani wa bei ya tani moja huwa ni Dola za kimarekani 400. Ili kupata thamani ya bei ya meli yote utazidisha na uzito wa meli ikiwa tupu (Lightship weight of the vessel). Biashara hii ya kukata meli umuingizia mhusika faida asilimia 69 na asilimia 2 huwa katika gharama za kulipa vibarua.



NAMNA MELI INAVYOKATWA

Meli husogezwa mpaka ufukweni kwa kuendeshwa kipindi maji yamejaa sana na kusogezwa kwa nguvu mpaka nchi kavu kwa speed kubwa, zoezi ili hufanyika na nahodha mzoefu meli huenda kukita sehemu ya ufukwe baada kutoka majini.

Kabla ya zoezi la ukataji kuanza mamlaka mbalimbali hufika kukagua na kutoa kibali, watu wa mazingira na watu ushuru na forodha. Zoezi la kwanza ni kutoa mafuta,oil,hydraulic na maji taka pia vifaa vya uzimaji moto na uokoaji uweka kwa tahadhari yoyote. Baada ya hapo zoezi la ukataji meli huanza kwa kutumia gesi na mashine za kukata vyuma vizito.

OIP.1uPH2E1Y1tmWsBoAaVx6lgHaDt



HATARI ZA UKATAJI WA MELI KWA WAFANYAKAZI

  • Harufu ya kemikali za asbestos . Material ya asbestos yakivutwa na mwanadamu yanaweza kumletea athari katika mfumo wa upumuaji na sehemu za meli kama kwenye engine, generator na boilers hutumia material ya asbestos kuzungushia bomba za joto.

  • Hatari ya kuangukiwa na vyuma vizito. Wakati wa kukata vyuma hutumia majukwaa kwa ajili ya kufikia sehemu za juu na kuna kuwa na hatari ya kuangukiwa na vyuma kwa walioko chini.

  • Kuungua wakati wa ukataji wa vyuma. Vyuma vizito hukatwa na gesi na machine nzito za kukatia moto, kutokana na uimara wa chuma hupelekea kutokea moto kutokana na msuguano.

UCHAFUZI WA MAZINGIRA
Baadhi ya mafuta kutoka kwenye matanki yasipotolewa yote hupelekea uchafuzi wa mazingira na maji ambayo viumbe maji huathirika.Oil, hydraulic na uchafu wa maji taka huingia baharini. Kemikali mbalimbali kutoka kwenye mitambo ya uzimaji moto wa meli.
Mwaka 2012 jumuiya ya Ulaya wao waliweka azimio na kutangaza kuwa meli zinazotakiwa kukatwa ni zile zilizo sajiliwa kwenye jumuiya ya Ulaya tu kupunguza uchafuzi wa mazingira.

OIP.iXcocY4Q_5Yn6ElZ7O2IsAHaE7
 
Hapa bongo Hadi izame yenyewe ,, maana kwa bongo sijawahi ona ndege imestaafu kazi

Ni Hadi ife

Huko mambele ndege nzima inaruka Safari yake ya mwsho baada ya hapo inaenda makaburini
 
 
Back
Top Bottom