Ship Stabilizer System

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Stabilization System ni mfumo maalum Kwenye chombo Cha majini Ili kukipa usawa kikiwa Kwenye Hali ya kutembea, bandarini au kikielea juu ya maji.

Stabilizer Kwa lugha rahisi ni sawa na suspension system katika magari. Kwenye meli ship stabilizer husaidia kupunguza chombo kuyumba sababu ya mawimbi au upepo mkali na kuleta utulivu katika chombo. Hizi husaidia kupunguza Hali ya abiria kujisikia vibaya wawapo majini(Sea Sickness) na kutapika wakati wa safari.

Aina za Ship Stabilizer
Ship stabilizer zinawekwa katika makundi makuu mawili ambayo ni Passive Stabilizer na Active stabilizer.

1.Passive Stabilizer
Passive Stabilizer ni Zile ambazo haziitaji mfumo wa Umeme au nguvu ya ziada Ili zifanye kazi zinapokutana na changamoto. Mfano ni Ballast Tanks haya ni matenki ambayo yapo sehemu ya Chini ya meli za mizigo na hujazwa maji au kupunguza maji Ili kuleta stability Kwenye meli.






Passive Fin Stabilizer
Kwenye Ngalawa za kuchonga pembeni zilikuwa zinaweka mbao kusapoti uzito upande wa kulia na kushoto. Passive Fin Stabilizer hizi hufungwa upande wa chini pembeni ya meli hufanya kazi ya kupingana na kuyumba au mjomgeo tofauti Kwenye meli Kwa kusogea taratibu bila kutumia nguvu au nishati ya ziada.



2.Active Stabilizer
Hizi ni njia za kisasa za kuipa meli au boti stability ambazo huitaji nguvu ya ziada kama Umeme Ili iweze kufanya kazi. Huu mfumo unajumuisha computer,fins, interceptor, hydraulic system na battery au Umeme Kwa ajili ya kuoperate.

Gryoscope Stabilizer
Hii ndio stabilizer ya Zamani iligunduliwa mwaka 1852 na mfizikia wa Kifaransa Leon Foucault baada ya kufanya majaribio kuhusu mzunguko wa Dunia katika mhimili wake na akaja na Jina la gyroscope. Mwaka 1904 mwanasayansi wa kijerumani Herman Anschutz-Kaempte alitengeneza Gryoscope iliyoweza kuzunguka direction yoyote na ikawa msaada Kwenye technology ya autopilot na Kwenye vita ya pili ya Dunia meli nyingi zilitumia kifaa hiki.

Gyroscope imetengenezwa mithili ya tufe ambalo hujizungusha Kwenye mhimili na limeshikiliwa na kitu ila Lina uwezo wa kuzunguka uelekeo wowote na mhimili nao unazunguka bila kuathiri mzunguko. Gryoscope haipendelewi sababu inachukua eneo kubwa na gharama za kufunga ni kubwa.






Stabilizer za kisasa
Namna hizi stabilizer zinavyofanya kazi inapokuwa Kwenye Hali ya kuyumba Interceptor hutoa Taarifa Kwenye computer na computer inaleta uamuzi wakufanya kinyume na kile kitendo mfano meli ilikuwa inayumba Kwa kulala upande wa kulia nyuzi 2 Basi itarudishwa upande wa kushoto Kwa nyuzi hizo Ili itulie.

Baadhi ya active stabilizer ni Austral Motion Control Interceptor,Naiad Interceptor na Humphree Stabilizer System.

Hizi hutumika Sana kwenye Boti za Kifahari (Yatch), Speed Boat,Boat za Abiria na Vyombo vya kijeshi.

Baadhi ya boti zilizofungwa hizi Stabilizer za kisasa ni Kilimanjaro 7 inatumia Naiad Stabilizer Interceptor na Zanzibar 1&2 hizi Zina Humphree Stabilizer Interceptor.

Humphree ndio technology ambayo ufanisi wake ni Mkubwa Zaidi katika Ship Stabilizer.




Faida za Hii mifumo
Inaleta ustareheshaji wakati wa safari, Usalama wa chombo dhidi ya dhoruba,kuzuia Watu waliopo ndani kutotapika na kuifanya siku kuwa nzuri hata kama Kuna upepo Mdogo au mawimbi ya Hapa na pale.


Hasara za Hii mifumo
Ni gharama Kwenye kununua,Bei za kufunga Kwenye chombo Cha Zamani Zipo na inahusisha kugusa bodi (Hull) ya boti wakati wa kuifunga.
 
Ahsante sana mkuu kwa darasa. Ila naomba kuuliza kama ifuatavyo:

1. Ipi tofauti ya passive fin stabilizer uliyozungumzia pamoja na fin stabilizer kama active control device?

2. Kulingana na andiko lako hii mifumo ina faida katika kupunguza ship roll motions ila naona umezungumzia sea sickness wakati tafiti zinatuambia vertical accelerations (motions) huchangia kikubwa katika kuathiri human metabolism (sea sickness na human comfort) unaweza kufafanua zaidi kuhusiana na hili?

3. Parameters zipi hutumika kama vipimio kutokana na ship motions katika suala zima la human performance and comfort kwa boti za abiria?

4. Unafikiri kwanini wenzetu hutumia high speed passenger ferries katika safari zao ukilinganisha na ferries ulizotaja lakini bado idadi ya wanaoathirika na sea sickness ni ndogo ukilinganisha na kwetu? Kwa maoni yako unafikiri ni hatua zipi zinaweza kuchukuliwa katika kupunguza hizo athari?
 
1.Passive Fin Stabilizer Hii inakuwa fixed Kwenye boti ufanyaji kazi wake hautaji nguvu ya Umeme wa betri au generator. Active Fin Stabilizer zinahitaji nguvu ya Umeme Ili ziweze kufanya kazi.

2. Kwenye faida nimesahau kuweka kazi kubwa ya hizi ni kuzuia ship roll nimeweka faida ambazo zinatokana baadae ya ship roll kutokuwepo.
Upo sahihi kazi kubwa ya hizi ni anti rolling. Husaidia kuzuia effect zote za ship motions ikiwa stationary au Kwenye movement.

3.Urefu wa Meli na Ship Stability Booklet husaidia kujua ni aina ipi ya Active Stabilizer itumike, na watengenezaji wa active stabilizer Wanazo kulingana na urefu wa chombo. Kwa boti chini ya Mita 12 unashauriwa kuweka interceptor set 1 ambayo itafungwa nyuma. Kwa boti kubwa unafunga interceptor mbele na nyuma au katikati Ili kuongeza ufanisi Zaidi.

4. Wenzetu wanatumia high speed ferry ambazo zinatumia Active Stabilizer System za kisasa kama Humphree,Naiad na Astral Motion hizi Kwa Sasa ndio Zina ufanisi kuanzia 85% kulingana na ubora wa kifaa.

Sisi speed ferry za Kwenda Zanzibar nyingi zilikuwa zinatumia Gyroscope ila Kwa Sasa kuanzia Kilimanjaro 7 inatumia Naiad Stabilizer System na Zanzibar 1 na 2 Zina Humphree Stabilizer System.
Humphree Stabilizer System Kwa Sasa ndio kinara Kwa ubora wa Hali ya juu.

Ili kupunguza athari Inabidi kuhamia Kutumia Hii mifumo ya kisasa ingawa kufunga Kwenye chombo Cha Zamani gharama Zake ni kubwa sana.
 
Nmejifunza . Asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…