SI KWELI Shirika la Afya Duniani(WHO) lawatahadharisha mikate ya kuoka kuwa inasambaza COVID-19

SI KWELI Shirika la Afya Duniani(WHO) lawatahadharisha mikate ya kuoka kuwa inasambaza COVID-19

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Hivi karibu kumekuwepo na taarifa ya kuwataka watu kutokula vitafunwa kama vile mikate n.k kwa ajili ya kuepuka maambukizi ya CoronaVirus

Taarifa hiyo ili kupewa uhalali wake, iliambatanishwa na nembo ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa(WHO) imesambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ikidai watu wanaweza kuambukizwa kupitia vyakula hivyo

20221116_155333.jpg
 
Tunachokijua
Ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona uliisumbua dunia tangu mwishoni mwa mwaka 2019.

Wataalam wa Afya walishauri watu kutumia vitakasa mikono au kuosha mikono kwa maji tiririka ili kuzuia kusambaa kwa virusi hivyo.

Kwa sababu hiyo Machi 2020, ulizuka uvumi ulioanzia Facebook ambapo ujumbe uliokuwa na nembo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ulisambazwa ukisema kuwa bidhaa za kuokwa (Kama mikate) zinasambaza virusi vya Corona kwa kuwa haziwezi kuoshwa.

Post iliyokuwa na uvumi huo ilifutwa, hata hivyo uko ushahidi wa makavazi yake. Baada ya kufuatilia suala hili kwa mapana yake, JamiiForums imebaini kuwa Picha hiyo haikuwa sahihi, WHO hawakutoa ujumbe huo. Na hakuna ushahidi kuwa vyakula vya kuokwa vinasambaza virusi kirahisi.

Hata namna ya jinsi chakula kinavyofungwa hakina ushahidi wa kusambaza virusi vya corona. Shirika la Chakula na Dawa la Marekani lilisema ni kweli kuwa mtu anaweza kuata virusi kushika virusi kwenye sehemu yenye virusi na kupeleka usino, hata hivyo hiyo sio njia pekee ya usambaaji wa virusi.

Kituo cha Kupambana na Kuzuia magonjwa (CDC) kiliripoti kuwa uwezekano mdogo wa corona kusambaa kutoka kwenye vyakula ambavyo husafiriswa kwa siku kadhaa au wiki ambavyo hutunzwa kwenye moto au kwenye jokofu, kwa kuwa virusi vya corona haviwezi kuishi kwenye hali hiyo.
Back
Top Bottom