Shirika la Bima la Taifa kuingia barabarani kukagua bima za vyombo vya moto imekaaje?

Code01

Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
16
Reaction score
18
Habarini wadau, nimeona leo kitu cha kushtua kidogo, Shirika la bima la Taifa (NIC) wameingia barabarani wakishirikiana na Traffic kukagua bima za vyombo vya moto.

Hili jambo linakaaje kwa watu binafsi wanaotoa huduma hiyo? Mbona ni kama biashara yao itakuwa ngumu!?
 
Sababu kuu kuna bima fake nyingi sana barabarani. Traffic si rahisi kugundua. Hata akigundua anapewa rushwa yanaishia hapo.
 
Wacha vitu vya kutunga..

NIC ni mnufaika wa moja kwa moja yeye mwenyewe kujidai au ku act kama regulator ni conflict of interests na pia ule uhayawani tunaoukataa...

Hii haifai hata kidogo... Kama ana low sales atulie, wenye wanajua Insurance ni scheme ya kuwatajirisha wanakata bima ndogo kabisa...
 
Sidhani kama wapo kukamata wasio na bima labda kuwapa elimu na kuungana nao NiC nothing else. NIC hawawezi ingilia shughuli ya kipolisi.
 
Hivi kwa nini Bima ya Afya isiwe serikalini tu.Sio mashirika binafsi ili kusaidia malipo madogo mfano 4500 kwa mwezi kila mtanzania
 
Sidhani kama wapo kukamata wasio na bima labda kuwapa elimu na kuungana nao NiC nothing else. NIC hawawezi ingilia shughuli ya kipolisi.
Kwa nchi hii ilivyo sasa, wanaweza kweli kuingia barabarani kufanya huo upumbaf.

Plas na raia wasivyojua sheria, tayari inakuwa ni fursa.
 
Wacha vitu vya kutunga..

NIC ni mnufaika wa moja kwa moja yeye mwenyewe kujidai au ku act kama regulator ni conflict of interests na pia ule uhayawani tunaoukataa...

Hii haifai hata kidogo... Kama ana low sales atulie, wenye wanajua Insurance ni scheme ya kuwatajirisha wanakata bima ndogo kabisa...
Sijatunga mkuu, nimesimamishwa leo barabarani na Traffic then nikaongea na watu wamevaa ID za NIC, walichosema ni kwamba wanakagua kama Gari ina bima active.
 
Na wewe ukawasikiliza mkuu?
 
Sijatunga mkuu, nimesimamishwa leo barabarani na Traffic then nikaongea na watu wamevaa ID za NIC, walichosema ni kwamba wanakagua kama Gari ina bima active.
Mdau alikujibu kwa dhana uliyosema bima fake zimekuwa nyingi. Hakuna Bima feki inayoweza kusoma kwenye mfumo wa TIRA. Makosa ya kawaida yanayofanyika katika Bima ni Under cutting hasa kwa magari ya Biashara, na Mwenyejukum la kufuatilia hilo ni TIRA na sio NIC maana hata wao Wanafanya makosa kama hayo.
Hata mim nimeshuhudia sana NIC wakiingia barabaran na Maofisa wa Polis kwa lengo la kukagua watu wasio na Bima kuwakatia papo kwa papo, Kwa upande wangu naona halina afya kabisaa maana inaondoa Fair Competition katika soko la bima. La Sivyo uruhusiwe kwa kila Kampuni kufanya hivyo.
 
Ni traffic alinisimamisha mkuu tena nilivyosimama hata hakusogea sikua na namna zaidi ya kuwasikiliza tu
Dah, pole mkuu.. ila next day waulize uhalali wa wao kukagua Insurance na hayo mamlaka wametoa wap?
 
Wacha vitu vya kutunga..

NIC ni mnufaika wa moja kwa moja yeye mwenyewe kujidai au ku act kama regulator ni conflict of interests na pia ule uhayawani tunaoukataa...

Hii haifai hata kidogo... Kama ana low sales atulie, wenye wanajua Insurance ni scheme ya kuwatajirisha wanakata bima ndogo kabisa...
Hili shirika limepitia nyakati ngumu sana hapo nyuma, hata sasa ni kama halijakua stable, ni kama ttcl flani hivi
 
Back
Top Bottom