DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Serikali inatumia jitihada kubwa sana kujenga vituo vya afya na kuhakikisha kwamba huduma hizi zinawafikia wananchi katika sehemu tofauti tofauti. Nakubali kwamba kuna umuhimu wa kuwa na miundombinu nchini lakini hilo ni jambo la kwanza tu. kinacho fuata ni kuhakikisha kwamba wananchi wana mudu gharama za matibabu na kupata afya bora.
Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na sinto fahamu kuhusu uwezo wa serikali kutoa huduma za afya bila gharama yoyote kwa wananchi au wananchi wote kuwa na bima ya afya bila kulipia michango yoyote. Ahadi hizi zote zinaonekana kuwa za uwongo haswa katika kipindi hiki ambacho shirika la bima ya afya Tanzania (NHIF) lina filisika.
Tujaribu kuangazia mapato ya NHIF ya kawaida na malipo yanayofanywa na shirika hili ili kuhakikisha kwamba walio jiunga na mpango huu wana nufaika. Njia kuu ya mapato kwa NHIF ni michango kutoka kwa wanachama wote walio chagua vifurushi tofauti tofauti kwenye mpango huu. Kama ilivyo bima zingine, malipo hufanywa bila ya mchangiaji kufahamu kama ataugua au la.
Ikitokea umechangia kwa muda hata wa miaka kumi bila kuugua basi fedha yako itakuwa kama faida kwa NHIF. Ila ikitokea kwamba umeugua, bima yako itaku gharamikia matibabu kulingana na kifurushi ulicholipia. Vilevile NHIF hulipia matibabu baada ya kuhakikisha kwamba kweli unaumwa. Hili hufanyika baada ya aliyeugua kutembelea hospitali inayopokea bima ya NHIF na kumuona daktari.
Je shirika la NHIF huwalipia wagonjwa matibabu kwa njia ipi?:
Hospitali zinazopokea bima ya NHIF hupeleka fomu za matibabu na dawa kwenye shirika la NHIF kila baada ya kuwa hudumia wagonjwa walio lipia bima hii. Malipo hufanywa moja kwa moja kwa hospitali husika kulingana na huduma ambazo wagonjwa hupata. Hii ina maanisha kwamba fomu zikipotea basi hospitali husika haziwezi kupata malipo kamili kutoka NHIF na vilevile udangayifu kwenye ujazaji wa fomu hizi husababisha hasara kwa shirika la NHIF.
Hospitali hugharamikia matibabu ya wagonjwa kwa kuhakikisha kwamba wanawalipa watumishi wa afya wote wano hudumia wagonjwa wa NHIF, kuhakikisha kwamba vipimo vyote vinafanya kazi na kuhakikisha kwamba dawa zote zinapatikana kwenye famasi zote zinazo hudumia wagonjwa wa bima ya afya.
Ikitokea kwamba dawa hazijapatikana hospitalini, wagonjwa huandikiwa fomu ambazo huwa wezesha kupata dawa hizi kwenye famasi ambazo hazipo hospitalini. Kwasababu hiyo, NHIF hufanya malipo kwa hospitali zote na famasi zote zinazo wahudumia wagonjwa wenye bima hiyo.
Shirika la NHIF kufilisika ina maanisha kwamba watu wote walio jiunga na bima hii hawataweza kupata huduma za matibabu kwenye hospitali husika na kwenye famasi zilizopo nje ya hospitali. Kama miezi miwili au mitatu iliyopita, NHIF walisitisha huduma ya kupata dawa kwenye famasi zilizo nje ya hospitali kwa tuhuma za kwamba kila mgonjwa lazima apate dawa zote hospitalini. Labda hii haikuwa sababu ya msingi na badala yake ni kupungukiwa kwa uwezo wa shirika hili kulipa famasi zilizo nje ya hospitali.
Nini kinaweza kufanya shirika hili kuweza kumudu kuwa hudumia watanzania kama kawaida?: Kwanza kabisa ni muhimu kuelewa kwamba hospitali zote zinatakiwa ziweze kuhudimia wagonjwa wote wa NHIF bila kutegemea mafungu kutoka serikalini kila mwaka. Malipo kutoka NHIF yanatakiwa kuziwezesha hospitali zote kuendesha mfumo huu vizuri.
Vilevile, udanganyifu kwenye ujazaji wa fomu hospitalini na kwenye famasi zote zilizo nje ya hospitali lazima utokomezwe. Kwa haraka haraka inawezekana kwamba shirika la NHIF linadaiwa fedha nyingi sana na hospitali mbalimbali pamoja na famasi binafsi. Kufilisika kwa NHIF kunaweza kumaanisha kwamba shirika hilo halina uwezo kulipa madeni haya na kwasababu hiyo lazima serikali iingilie kati ili kuhakikisha kwamba wananchi wanaendelea kupata huduma hii.
Ama kweli, bima ya afya kwa watanzania wote bado ni ndoto ya Abunuwasi.
www.mwananchi.co.tz

NHIF yatupiwa mzigo wa dawa
Baada ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kusitisha maboresho yaliyolalamikiwa na wanachama wake, kero kadhaa zimetajwa kuhusu mfuko huo, ikiwamo baadhi ya vituo vya afya kudai mfuko umekuwa...
Aliyekuwa mhasibu NHIF kortini, asomewa mashtaka 30
Aliyekuwa mhasibu msaidizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Mara, Francis Mchaki (37) amefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka 30 likiwemo shtaka la uhujumu uchumi na...
Nakisi yatishia uhai wa NHIF
Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imesema imebaini Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) unatengeneza nakisi katika mapato na matumizi, jambo ambalo linatishia uhai wa mfuko.
Magonjwa yasiyoambukiza yaikamua NHIF
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umesema fedha nyingi za mfuko huo zinatumika katika kushughulikia magonjwa sugu, huku dawa za saratani na huduma ya kusafishwa figo ‘dialysis’ nazo zikitumia...