Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kundi la Bunge la Morocco limependekeza mswada utakaowaruhusu wanawake kupewa siku za likizo ya hedhi yenye malipo.
Katika kile ambacho kitakuwa sheria ya aina yake kwa eneo la Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, pendekezo la kikundi cha haki za kijamii cha shirika la Bunge la Morocco, linalenga kuboresha hali ya wanawake kazini, kupitia utoaji wa likizo ya hedhi yenye malipo ya siku mbili.
Kulingana na mswada uliopendekezwa, wafanyikazi wa kike hawatahitaji kutoa ushahidi wa matibabu kila wakati wanapohitaji kuwa nyumbani.
Mswada huo hata hivyo unahitaji kujadiliwa na kuidhinishwa na serikali ya Morocco.
Wazo iwapo muswada huo utapitishwa, ni kuutekeleza kwa awamu, kuanzia kwa watumishi wa Serikali, ili kuona jinsi utakavyokuwa na ufanisi.
Viongozi hao pia wanaeleza kuwa hedhi ni mwiko ndani ya jamii na kwamba kundi hilo la wabunge linalenga kufungua mjadala kuhusu njia za kuondoa vikwazo vyote vinavyowakabili wanawake katika maisha ya umma.
Iwapo itapitishwa, Morocco itakuwa nchi ya pili barani Afrika, baada ya Zambia, kuwa na sheria hiyo.
Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ilipitisha sheria hiyo mwaka 2015, inayowaruhusu wanawake kuchukua siku ya mapumziko katika kipindi chao cha hedhi. Nchi nyingine zinazotoa likizo ya malipo ya hedhi ni pamoja na Korea Kusini, Japani, Taiwan na Indonesia.
Chanzo: BBC