Shirika la Msalaba Mwekundu lapigwa marufuku nchini Niger

Strong ladg

Senior Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
170
Reaction score
445
Mamlaka nchini Niger zimeliamuru shirika la msalaba mwekundu kusimamisha shughuli zake nchini humo na kufunga ofisi zake mara moja .Vilevile, Niger imevunja mikataba iliyoruhusu shirika hilo kuendesha shughuli zake nchini Niger.

Baada ya kupokea amri hiyo kutoka serikalini, ofisi zote za shirika hilo zilifungwa siku ya Jumanne ya tarehe 4 Februari 2025 na wafanyakazi wa shirika hilo ambao ni raia wa kigeni, walianza taratibu za kuondoka nchini Niger.

1738910376167.png
Ingawa sababu za serikali ya Niger kufanya hivyo hazikuwekwa wazi, inaaminika serikali ya kijeshi ya Niger imelihusisha shirika hilo na ufadhili wa vikundi vya kigaidi.

Itakumbukwa kuwa mwishoni mwa 2024 kupitia televisheni ya taifa ( RTN), serikali ya Niger ilitoa ripoti iliyoonyesha kuwa Ufaransa inafadhili shughuli za ugaidi nchini Niger kwa kushirikiana na mashirika ya misaada.

Niger iliapa kuyashughulikia mashirika yote yanayotumiwa na serikali ya Ufaransa kufadhili shughuli za ugaidi nchini humo.

Katika hatua nyingine, mwaka 2024 serikali ya Niger ilimfukuza balozi wa umoja wa Ulaya nchini humo baada ya Umoja huo kupeleka fedha kwenye mashirika ya kutoa misaada pasipo kuitaarifu serikali. Serikali ya Niger ilidai kuna uwezekano wa fedha hizo kuishia kwenye mikono ya magaidi.

==

The government of Niger announced the abolition of the headquarters agreement of the International Committee of the Red Cross (ICRC) and ordered it to close offices in the country and immediately evacuate its foreign employees, according to a verbal note dated Jan. 31.

A Nigerien civil society figure who works with the ICRC said it was the Ministry of Foreign Affairs that denounced the organization's headquarters agreement. Since the head of the ICRC has the rank of diplomat, a verbal note is enough to make the government's decision official.

According to local media, the ICRC received the note on Feb. 4 and published the results of its work in Niger during the first half of 2024 on its official website the same day.

The ICRC said in its report that it entered Niger in 1990, with offices in Diffa, Tillaberi and Tahoua; it provided medical services to 121,236 victims of armed conflicts in the first half of 2024.

To date, neither side has responded when asked to comment.
 
Sisi ndiyo kwanza tupo mikoni mwa raia feki💀💀💀Rostam akimwambia samia bushiri tukimbie watanganyika wametushitukia
 
Attachments

  • AQPzVoRs7BEeifpHw1ntGXCmpXnYr-2WpwP1ESLL_Canvf2s01Cnzy3Zc36VQu6U-ZcmRlh9LYD80RVTM3c7z_T5.mp4
    800.8 KB
Haya mashirika yanayojiita ya misaada au NGO actually ni majasusi yametumwa kwa kazi maalumu. Hapo wako kwa maslahi ya nchi zao na kamwe sio kutoa misaada. Ndio mana unakuta misaada yenyewe ni chandarua au pedi za wanawake; upuuzi mtupu
 
Afrika inawahitaji viongozi wenye uthubutu! Na siyo aina ya wale viongozi waaokubali kupandishwa kwenye basi la daladala, walipokwenda kushuhudia tukio la kusimikwa madarakani mfalme wa Uingereza.
Udhuhutu Gani hapo ushamba tu, ugaidi unafadhiriwa na nchi za kiarabu kama Irani na Qatar. Yemen na somalia Kuna ugaidi vipi Kuna red cross kule? Tuache ujuaji wakuu
 
Kwa hiyo Al Qaeda, ISIL, Mujahedeen wa Taliban, na vikundi vingine vingi vilianzishwa, na pia kufadhiliwa na nchi za Kiarabi kama Iran na Qatar! Ok.
 
Udhuhutu Gani hapo ushamba tu, ugaidi unafadhiriwa na nchi za kiarabu kama Irani na Qatar. Yemen na somalia Kuna ugaidi vipi Kuna red cross kule? Tuache ujuaji wakuu
Ufaransa imeshtakiwa kule Umoja wa Mataifa kwa kufadhili ugaidi nchi za Afrika Magharibi. Wanaweza kuwa wanahusika. Hujiulizi kwanini nchi zote zilizokuwa na magaidi zilikuwa na kambi za jeshi za wafaransa( with exception of Nigeria). Na inakuwaje wanajeshi wa Ufaransa wanakaa nchi fulani zaidi ya miaka na miaka wakisema wanapambana na magaidi lakini magaidi hawaishi. Jeshi la Ufaransa ni dhaifu kiasi hicho??
 
Sasa umeambiwa somalia hakuna Red cross...soma hiyo habari vzr ilivyo andikwa serikali ya Niger ndo imegundua huo mlenyezo wa pesa unapitia kwny mashirika ya nje hasa Ufaransa...sasa unataka kupingana na uchunguzi wao?...au unaleta ugalatia wako kila jambo linalohusu msalaba?..mbn msalaba huo huo watu wanaucgezea porno na kawaida tu
 
Ufaransa imeshtakiwa kule Umoja wa Mataifa kwa kufadhili ugaidi nchi za Afrika Magharibi. Wanaweza kuwa wanahusika. Hujiulizi kwanini nchi zote zilizokuwa na magaidi zilikuwa na kambi za jeshi za wafaransa( with exception of Nigeria). Na inakuwaje wanajeshi wa Ufaransa wanakaa nchi fulani zaidi ya miaka na miaka wakisema wanapambana na magaidi lakini magaidi hawaishi. Jeshi la Ufaransa ni dhaifu kiasi hicho??
Ni kama DRC; vikosi ya UN vipo hapo zaidi ya miongo miwili ila VURUGU NDIO ZINAZIDI. Hao wanaoitwa wafadhili ni MASHETANI SANA. MIPANGO YAO NI KUVURUGA AMANI NA KUIBA RASILIMALI ZILIZOPO KWA KUTUMIA VIBARAKA WAO AMABO WENGI NI VIONGOZI WA AFRIKA NA VIONGOZI WA VIKUNDI VYA MAGAIDI/WAAASI
 
Case study ni Congo.

Africa inahitaji viongozi type hi ya huyu wa Niger, Mali, Bukinafaso, yule wa Zambia (though now days ni kama kapoa poa hivi ) halafu angekuwepo na JPM hapa Tanzania, bara lingechangamka; wazalendo kweli kweli hawa watu.
 
Ni kama DRC; vikosi ya UN vipo hapo zaidi ya miongo miwili ila VURUGU NDIO ZINAZIDI. Hao wanaoitwa wafadhili ni MASHETANI SANA. MIPANGO YAO NI KUVURUGA AMANI NA KUIBA RASILIMALI ZILIZOPO KWA KUTUMIA VIBARAKA WAO AMABO WENGI NI VIONGOZI WA AFRIKA NA VIONGOZI WA VIKUNDI VYA MAGAIDI/WAAASI
Nchini Mali, magaidi walipungua punde tu baada ya vikosi vya UN kufukuzwa. Siku wanafungasha virago,waziri wa mambo ya nje wa Mali aliwachamba kwelikweli bila kupepesa maneno. Natamani kila mtu angeipata ile hotuba wakati UN wanapewa makavu. Hao watu sio wazuri.
 
Back
Top Bottom