Naona kama vile vifurushi wanavyopitisha pale hata mishahara yao havitoshi kuwalipa....
Wamepewa mkongo wataifa hata hakuna mkoa mmoja wanaweza kuutoa kama mfano r
Kwa sasa hivi tozo zao za vifurushi + kodi za zinaendana na kina DHL/UPS wakati hao washindani wapo mbali sana kwa technologia, na usalama
Ushauri;
1. Deni analipiwa anayezalisha, sasa kama wanachozalisha hakitoshi hata kujiendesha, unalipa deni ili watengeneze deni jingine?
2. Wabunge waje na mkakati rasmi wa kuifufua posta kwa kuweka kodi rafiki kwa parcel za kawaida. Mfano mtu alipie gharama za posta + 18% basi.. kwa tozo zilizopo kwa sasa, sioni wakiweza kushindana na private competitor DHL, na wengine (hawafiki mahali)
3. HAWANA UBUNIFU wa kusogeza huduma karibu na watu (kwenye stand zote kubwa za mabasi, viwanja vya ndege nk. wao ndio walitakiwa wapokee bighaa wazitume kwa mabasi lakini ndio hivyo tena....
4. Wabinafsishe ili Sector binafsi iwasaidie kuendesha