Shirika la Posta lifutwe, limejaa uhuni

Shirika la Posta lifutwe, limejaa uhuni

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari waungwana!

Naomba kuelezea kwa ufupi juu ya hujuma/ uhuni unaofanywa na wahudumu wa posta baadhi ya matawi.

- Wahudumu wanawalazimisha watu watume barua kwa njia ya EMS. Ninaposema kulazimisha namaanisha hawakushikii bunduki bali wanakwambia hii ndio njia ya haraka, wakikuona unajua taratibu wanakwambia barua isipofika usinilaumu.

Hivi kwa mfano tangazo la kazi limetolewa Dar es Salaam na mwajiri hajalazimisha utumie EMS kuna ulazima gani kumfosi mtu atumie njia ya EMS huku na yeye yuko hapahapa Dar es Salaam na deadline ni siku 12 mbele?.

Nimewahi kutumiwa kifurushi(kopi za vyeti) kutoka Lindi kwa njia ya EMS nilikipata kifurushi baada ya kupita wiki moja tena walinitaka nikifuate Mimi mwenyewe posta mpya badala ya wao kuniletea au kuniwekea kwenye box langu. Hapo kuna umuhimu gani wa kutumia hii njia ya ems ambayo ni expensive na tunaambiwa ni ya haraka?.

-Kuna rafiki yangu yuko wilaya moja hivi huko Lindi alipeleka barua posta aitume Dar wanamwambia atumie EMS, alipomwambia mhudumu njia ya kawaida anaambiwa itachelewa na inabidi atumie 6000 sh. While ems atumie 15000.

Hata kama una vyeti vingi kama Professor na uweke na vyeti vya ndoa pamoja na kipaimara huwezi kutumia stamps za SH.6000.

TPC hebu wachunguzeni wahudumu wenu.

Huenda mmewapa mpango kazi wa kukusanya kiwango fulani annually na wao wanatumia kila njia ikiwemo kuwasukumia watu kwenye EMS ili kufikia lengo. Au wanajiongeza ili wapate ridhiki (embezzlement).

Dunia inabadilika, serikali kuna umuhimu wa kuondoa haya mashiklrika au kuyaboresha maana hii mifumo ya monopoly ishaisha muda wake.
 
Hivi kwanini systems za serikali yetu ni zakizamani sana yaani hawaendi sambamba na dunia kabisa, tunapitwa na nchi ndogo kama kenya duh! Ukienda BOT majanga zaidi hawaruhusu PAYPAL, ukija TCRA utakuta sheria kandamizi za kibeberu za kulipishwa youtube, ukija TANESCO Ndo madudu hatari, ukienda TRA BANDARINI ndo utalia aisee!!mzigo wa 10,000Tsh unalipishwa 50,000 Tshs, hao posta ndo usiseme wakiona mzigo mkali wanasepa nao kimya kimya. Are these guys serious? 😤😡


Rais mwenye exposure ndo anahitajika hapa kama Kagame.
 
Hivi kwanini systems za serikali yetu ni zakizamani sana yaani hawaendi sambamba na dunia kabisa, tunapitwa na nchi ndogo kama kenya duh! Ukienda BOT majanga zaidi hawaruhusu PAYPAL, ukija TCRA utakuta sheria kandamizi za kibeberu za kulipishwa youtube, ukija TANESCO Ndo madudu hatari, ukienda BANDARINI ndo utalia aisee!! 😤😡


Rais mwenye exposure ndo anahitajika hapa kama Kagame.

tatizo ni CCM ndugu
 
Kwa maoni yangu mi nadhani shirika hili inabidi lifumuliwe upya, uwekwe muundo wa kisasa wa utendaji na uendeshaji, lipewe mtaji wa kutosheleza investments mbalimbali kwa sababu lina network kubwa na mtendaji mkuu wake apewe targets za kufikia mfano ndani ya miaka mitatu sales turnover ipande kwa asilimia 60 na afuatiliwe. Kwa staili hii naamini shirika litasogea mahala
 
Hivi kwanini systems za serikali yetu ni zakizamani sana yaani hawaendi sambamba na dunia kabisa, tunapitwa na nchi ndogo kama kenya duh! Ukienda BOT majanga zaidi hawaruhusu PAYPAL, ukija TCRA utakuta sheria kandamizi za kibeberu za kulipishwa youtube, ukija TANESCO Ndo madudu hatari, ukienda TRA BANDARINI ndo utalia aisee!!mzigo wa 10,000Tsh unalipishwa 50,000 Tshs, hao posta ndo usiseme wakiona mzigo mkali wanasepa nao kimya kimya. Are these guys serious? 😤😡


Rais mwenye exposure ndo anahitajika hapa kama Kagame.
Very childish and pain joke
 
Juzi yule muhumu ashukuru wale askari ningempasua wanatia hasira sana


It is never too late to begin. Start now
 
Bongo hata lodge uaminifu hamna
Nimepoteza vitambulisho vyote muhimu sababu ya uzembe wa wahudumu wa guest house na polisi hata kuniandikia Loss report wanataka vipimo vya corona.😬😬😬😬😬
 
Kuna mdau kasema tatizo ni "monopoly". Pigia mstari hapa, na shida inaanza na "monopoly structure" kwenye siasa tuliyonayo!
 
Kuna umuhimu wa kuaajiri wageni kwenye mashirika yetu ya umma maana wabongo wamezidi uwizkid
 
Back
Top Bottom