Mganguzi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2022
- 1,604
- 3,715
Wazee wetu waliolitumikia shirika la reli Tanzania kwa jasho na damu asilimia kubwa kwa sasa wamepoteza maisha na wengine wako hoi vitandani na ama wako hoi kimaisha! Serikali kupitia shirika la reli TRC wanatangaza mafanikio ya SGR na kununua vichwa vipya vya train za kisasa na kujenga reli mpya juu ya laana ya machozi ya wazee Hawa !
TRC ni shirika lenye dharau kubwa kwa wastaafu haijapata kutokea ! TRC ni matapeli wa haki za wafanyakazi wao waliostaafu kwa miaka na miaka ! TRC hawana pesa za kuwalipa makomredi Hawa walioendesha hili shirika kwa tabu na kwa mifumo migumu lakini wanapesa za kununua vichwa na mabehewa mapya !
Nimekutana na mzee magelanga syprian 88 akiwa hoi kitandani anadai amefuatilia stahiki zake mpaka sasa ameamua kumuachia Mungu! Watoto hawana pesa ya kumuuguza Wala makazi ya kuishi ilihali analidai shirika zaidi ya mil 144, kwa nini TRC mmekuwa na roho mbaya kiasi hiki ?
Kwanini TRC hamuogopi kukalia jasho la watu? Kwanini TRC mmebaki na fedha za watu mpaka wamekufa na familia zikifuatilia haki zao mnawapiga danadana mpaka wakate tamaa !!
TRC chini ya Masanja Kadogosa mnaweza kuieleza jamii ya watanzania dhamira yenu ni ipi kama sio utapeli wa jasho la watu ? Tuseme ni TRC ama tuseme ni Masanja Kadogosa? Au mnawapiga danadana ili wafe mjilipe wenyewe? Mnafanya makusudi kwa kuwa mnatembea juu v8 hamkanyagi chini ? Vipi mzazi wako wewe Masanja Kadogosa angekuwa anadai usingemlipa? Na wewe ukistaafu utajisikiaje usipolipwa kwa zaidi ya miaka 20!
Laaana iwe juu yenu nyinyi wote mnaokalia mafaili ya wastaafu bila huruma ,Mungu ilaani TRC !!