Shirika la Reli (TRC) lifumuliwe

Enkaly

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2014
Posts
307
Reaction score
428
Shirika la Reli kwa kweli ambalo ni shirika mama kwenye sekta ya usafirishaji linatia aibu.

Shirika lina MATITI kila kona, getini na ndani ya train lakini cha kushangaza uendeshaji wake hauridhishi hata kidogo.

Viongozi wapo, wabunge wapo, mawaziri wapo hawayaoni haya? Wanafanyaga ziara za kwende nchi zingine kufanya nini kama hata kile kidogo kisichohitaji pesa kinatushinda?

Hivi karibuni treni lilitoka Dar kwenda Kigoma, abilia walikwama Dodoma siku mbili, hakukua na taarifa yoyote ya msingi. Then tunataka maendeleo ya aina gani bila kuwa na mfumo wa kujali muda? Kama wataalam serikali inawasomesha mwisho wa siku wataalam hao hao hamwaajili, wanaishia kufanya shughuli zingine ambazo sio taaluma zao. Tatizo ni nini?

Hakuna mfumo wa kujali mteja kabisa.

Leo tumepanda treni saa kumi na mbili kasoro, treni la DAR - PUGU hakukua na taarifa yoyote kwa abilia. Ambapo kawaida saa12:05 jioni linatakiwa lianze safari, lakini siku hizi hakuna taarifa yoyote kwa wateja wake, tunakuja kuondoka saa moja usiku.

Kimsingi viongozi husika wajaribu kulichunguza suala hili linakela sana kwetu sisi abilia wa Pugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…