Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulika na Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) limesema Nusu ya mimba duniani kote hazikutarajiwa

Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulika na Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) limesema Nusu ya mimba duniani kote hazikutarajiwa

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Ripoti ya Hali ya ldadi ya Watu Duniani mwaka 2022, iliyotolewa Machi 30, 2022 na Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulika na Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) imeonyesha kuwa karibu nusu ya mimba zote ambazo ni jumla ya milioni 121 kila mwaka duniani kote, hazikutarajiwa.

Ripoti hiyo iliyopewa jina la "Kuona yasiyoonekana: Kuchukua hatua katika janga lililopuuzwa la mimba zisizotarajiwa," ilizinduliwa jijini New York, Marekani na imeeleza kuwa waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana, kwani iwapo wanataka kuwa na ujauzito au la huwa si chaguo lao binafsi.

Asilimia 60 ya mimba hizo zinaishia kutolewa na kati ya hapo asilimia 45 haitolewi katika njia salama, asilimia 5 hadi 13 wanapoteza maisha.

"Ripoti hii ituamshe kutoka usingizini. ldadi kubwa ya mimba zisizotarajiwa inaonesha kushindwa duniani kote kutetea haki za kimsingi za wanawake na wasichana," alisema Mkurugenzi

Mtendaji wa UNFPA, Dk Natalia Kanem.

Source: United Nations Population Fund (UNPF)
 
Back
Top Bottom