Wangeunda upya TFDA iwe inashughulikia kila kitu, ubora wa bidhaa na vinywaji na udhibiti wa bidhaa za kutoka nje.
TBS ivunjwe.
Kisha ili kuondoa usumbufu kwa raia kuzunguka kutafuta vibali na kujisajili iundwe tovuti wa ajili ya wafanya biashara kuitumia popote pale walipo.
Kwa kuwa tayari BRELA na TRA wapo zile kanzi data zinakuwa zinawasiliana mtu anapotaka vibali ili kufanya uhakiki.
Mtu akimaliza kila kitu mtandaoni ndo aenda kule ofisi za TFDA kuhakiki na kukabidhiwa vibali original.
Hayo yatakuwa ni mapinduzi ya kimaendeleo pia si tu kufukuzana na akina nanihii.