Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wadogo kuchangamkia fursa ya kushiriki Tuzo za ubora

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wadogo kuchangamkia fursa ya kushiriki Tuzo za ubora

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) imewataka wafanyabiashara na watoa huduma wakubwa na wadogo kuchangamkia fursa ya kushiriki Tuzo za ubora kwenye huduma na bidhaa.

Ndugu Baraka Mbajije (Afisa udhibiti ubora - TBS) amesema lengo la Tuzo hizi ni kuhakikisha kuwa mifumo ya bidhaa na huduma zinakidhi ubora kitaifa, kikanda na kimataifa na hivyo kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote.

Pia Baraka Mbajije amesema "tuzo hizo ni sehemu ya mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinazotengenezwa nchini kupitia matumizi ya viwango na kanuni za ubora kwa taasisi za umma na binafsi"

Pia ndugu Salim Mohamed (Afisa Viwango - TBS) Amesema tuzo hizo zimegawanyika katika vipengele vitano ambavyo ni:-

▶️Tuzo kwa kampuni bora ya mwaka,

▶️ Tuzo kwa bidhaa bora ya mwaka,

▶️ Tuzo huduma bora ya mwaka,

▶️ Tuzo kwa muuzaji bora wa bidhaa nje ya nchi

▶️ Tuzo ya mtu mmoja mmoja aliyefanya vizuri kwenye masuala ya ubora.

“Kwa kipengele cha kwanza hadi cha nne zimeandaliwa tuzo kwenye makundi mawili kwa kila kipengele yaani tuzo kwa kampuni kubwa na pia tuzo kwa wajasiriamali wadogo na wakati" - ndugu Salim Mohamed Ameyasema hayo katika Mkutano na Waandishi wa habari.

Ndugu Salim Mohamed amesema wadau wote wanaotaka kushiriki basi watembele katika tovuti rasmi ya TBS (www.tbs.go.tz) watakuta link ya Jinsi ya kushiriki na Mwisho wa kutuma Maombi ni Tarehe 17 NOVEMBA, 2022

FB_IMG_1668155414412.jpg
 
Back
Top Bottom