Shirika liliridhikaje na Kiswahili hiki cha Kuomba Kazi?

Shirika liliridhikaje na Kiswahili hiki cha Kuomba Kazi?

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Shirika moja kubwa la hifadhi ya jamii limetengeneza tangazo la kusifia huduma zake.
Tangazo liko hivi: Mtu mmoja anaingia kwenye nyumba asiyoijua vizuri, na mara anamkuta mwenye nyumba ambaye anamwuliza mgeni: 'Unataka nini?
Jibu:Nilitaka nipate kazi.
Hivi kweli, wanaotafuta kazi ndivyo wanavyosema?
Mimi nafikiri wanaotafuta kazi husema:Naomba kazi kama ipo.
Na huyu kwenye tangazo kwa kuwa ameingia nyumbani kwa mtu ambaye hajatangaza nafasi yoyote ya kazi, angesema: Naomba kazi yoyote kama ipo. Lakini eti, nilitaka nipatee kazi.
Kama umelisikia hilo tangazo utakubaliana namikwamba lugha iliyotumika si sahihi.

Hata hivyo kwa kuwa ni tangazo linaisha kwa mtafutaji kupewa kazi na kusema yale ambayo shirika lilitaka yasemwe kwa kujitangaza.
 
Back
Top Bottom