RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (67)✍️
Kuna msemo unasema "ukitaka kufika haraka nenda peke yako, lakini ukitaka kufika mbali nenda na wenzako." Kupitia msemo huu unadhihirisha kwamba ili ufike mbali hupaswi kujitenga sana. Kwenye safari yako ya mafanikio watu ni muhimu sana, na wala hupaswi kuogopa adui.
Acha kiburi. Kama ulimkosea mzazi, rafiki, ndugu, au watu wengine omba msamaha ili uzidi kufungua milango yako ya baraka. Hata wafanyabiashara wakubwa duniani wanahitaji watu (wateja), na hawapendi kuchafua brand yao kwa watu.
Ukihisi umewakosea watu usijipe kiburi kwa kusema wewe ni jeshi la mtu mmoja. Hakuna nchi ambayo ina Jeshi la mtu (askari) mmoja, hebu shirikiana na wenzako.
Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Shirikiana na wenzako katika matukio ya misiba, sherehe, biashara, elimu, na matukio mengine ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ili ufike mbali.
RIGHT MARKER
DAR ES SALAAM