Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), linatarajiwa kumaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda wa siku 12

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA), linatarajiwa kumaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda wa siku 12 jijini Lisbon-Ureno, mwezi Agosti mpango ambao utaamuliwa leo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ya UEFA .

Hatua za robo fainali, nusu fainali na fainali zitachezwa jijini Lisbon kuanzia tarehe 12-23 Agosti huku timu zilizosalia kucheza mechi za marudiano hatua ya 16 bora kama Chelsea na Bayern Munich na Manchester City na Real Madrid kusemekana kuchezwa kwenye Viwanja vyao binafsi.

Mpango huu umependekezwa kwa ajili ya kumaliza mashindano mapema kuliko kucheza kama kawaida nyumbani na ugenini, mfumo huu pia utatumika kumaliza mashindano ya Europa nchini Ujerumani.
 
Washapitisha,16 bora itachezwa 7/8 August na robo,nusu na fainali itachezwa Lisbon. Huku robo na nusu fainali itakuwa ni match moja tuu umeng'oka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…