Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Kim Poulsen kuwa Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
22,719
Reaction score
40,739
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Kim Poulsen raia wa Denmark kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars)

- Poulsen anachukua nafasi ya Kocha Ettiene Ndayiragije ambaye mkataba wake umevunjwa.

Alishawahi kuwa Kocha wa Taifa Stars (2012-2014)

 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Kim Poulsen, Raia wa Denmark kuwa Kocha Mkuu mpya wa Taifa Stars,

Poulsen ambaye amewahi kuwa Kocha wa Taifa Stars (2012-2014) anarithi nafasi ya Etienne Ndairagije, Raia wa Burundi.
 
Timu yetu hii tatizo si kocha,ila michezaji tu haijitambui
 
Hao kina Paulsen wapo wawili.
Kuna yule mmoja alikua anafundisha Taifa stars na mwingine alikua Serengeti boys, na baadae akaja kufundisha Taifa stars.

Sasa ni yupi kati yao alie rudi?

Binafs kama karudi yule alienza kufundisha Serengeti boys, tume pata bonge la kocha.

Hapa kula matapishi yetu sio kosa.

Lakini akiwa yule babu alie kua akifundisha Taifa stars, hapo tumejichanganya.
 
Kuna viongozi wananufaika na hii mikataba ya hawa makocha wa timu za taifa.
 
Kim Paulsen ni yule aliyekuwa akiwafundisha Serengeti Boys! Na baadae akafanywa kimy kimya kuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF. Kile kibabu kilicho kuja na huyu Kim kinaitwa Jan Paulsen.

Huyu ndiye aliyemfanya Oscar Milambo kuonekana ni bonge la Kocha! Ila baada ya kufanyiwa figisu na kuondoka nchini, tunakumbuka na huyo Oscar Milambo alivyo kuja kumbwela wakati timu ilipokuwa mwenyeji wa Afcon U17.
Akipewa muda, atafanya kitu. Huyu jamaa amebobea sana kwenye soka la vijana.
 
mpira bongo ulionekana kipindi cha maximo, arudishwe tafadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…