maoni yangu ni kwamba wana tanganyika wanaitaka tanganyika yao, shivji na wenzake wanaotaka kuififisha hoja hiyo kwa vitisho dhaifu kama gharama za uendeshaji na uwezekano wa kuvunjika muungano wafanye hivyo wakijua kuwa watanganyika hawawezi kudanganyika kiurahisi kiasi hicho, kuhusu gharama ni wazi kondoo hawezi kushindwa kubeba mkia wake, vile vile tanganyika haiwezi kutolewa kafara au kuwa held hostage kwa lengo la kuuponya muungano usio na sababu za msingi ukiachilia suala la kuoleana. Lakini vile vile heshimuni kodi za watanganyika na wazanzibar zilizotumika kwenye ukusanyaji maoni kwa kuzingatia maoni yaliyotolewa na walio wengi, haya yasipofanyika jibu mnalo kwamba hata polisi wakipiga wananchi kama walivyoamriwa na pinda na kulazimisha kupitishwa kwa mawazo ya wachache katika serikali, vuguvugu la kudai tanganyika litaendelea kuwa political battle cry ya watanganyika mpaka litakapokuwa realized, ndiyo, mchakato wa kuidai tanganyika waweza kuwa costly hata kusababisha watu wengi kuumizwa na hata kuuawa lakini ni wazi kwamba ndoto ya kuwa na serikali ya tanganyika inastahili kulipiwa gharama za kutosha kwani ni ndoto tamu.:angry: