SHIVYAWATA: Mafuta ya Ualbino yaondolewe kundi la vipondozi

SHIVYAWATA: Mafuta ya Ualbino yaondolewe kundi la vipondozi

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wanachama wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wameiomba serikali kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kutambua mafuta yanayotumiwa na watu wenye ualbino kama tiba badala ya kuyajumuisha kwenye kundi la vipodozi, kama ilivyo sasa.

Ombi hilo limetolewa na Mohamed Charles wakati wa Mkutano wa Kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, uliofanyika Desemba 15, 2024, katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam. Mohamed amesema kuwa gharama ya mafuta hayo ni kubwa kwa sababu ya kujumuishwa kwenye kundi la vipodozi, hali inayowafanya watu wenye ualbino kushindwa kumudu mahitaji yao ya mafuta hayo muhimu.

Mafuta yanayotumiwa na watu wenye ualbino yanahitajika kwa ajili ya kuwakinga dhidi ya athari za mionzi ya jua, ambayo inawaweka katika hatari kubwa ya saratani ya ngozi. Mohamed amesisitiza kuwa mafuta hayo si bidhaa za anasa, bali ni mahitaji muhimu ya kiafya kwa watu wenye ualbino.

 
Back
Top Bottom