Kitendo cha Mshambulizi Shizya Kichuya cha kufunga goli na kukimbilia ilipo picha ya Mafisango si tu kimeonesha mapenzi ya dhati ya mchezaji huyo kwa Klabu yake lakini pia kuonesha jinsi alivyo na kiu ya kuigeuza mioyo ya wanamsimbazi kwamba huenda akaziba kiu yao na pia kuwaenzi wachezji waliotumika kwa mafanikio makubwa klabuni hapo na pia kimetoea tafsiri ya yeye kuvaa NAMBA 25 pia
huyu ni mmoja ya wachezaji waliojituma sana mechi ya AZAM VS SIMBA
Mo ameahidi kutoa Sh milioni 10 ambayo itaongezwa na milioni 10 nyingine ambazo hutolewa na wanachama kwa kujichangisha na kufanya bonus ifike Sh milioni 20.
Fedha hizo zitakabidhiwa kwa wachezaji ikiwa watashinda pambano hilo dhidi ya Azam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam, lengo la kufanya hivyo ni kuongeza morali ya ushindi kwenye pambano hilo.