Shomary Kapombe ndiyo Mchezaji Bora Simba kwa sasa

Shomary Kapombe ndiyo Mchezaji Bora Simba kwa sasa

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kama umefuatilia uchezaji wa Shomary Kapombe toka amepona majeraha yake amekuwa anacheza kwa kiwango kikubwa na kujituma kuliko mchezaji yoyote pale Simba.

Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, ni kama game moja tu ndiyo kidogo alikuwa na changamoto uwanjani.

Kama kuna mchezaji wa Simba alistahili udhamini kama ule wa CRDB basi ni Shomary Kapombe.
 
1.Mimi kwangu ni Inonga japo ameshuka kidogo.
Inonga anaibeba sana Simba.

2. MZAMIRU akiamua kukichafua, ila anapoteza sana pasi.

3. Kapombe japo maji (majaro) yake hayana faida
 
1.Mimi kwangu ni Inonga japo ameshuka kidogo.
Inonga anaibeba sana Simba.

2. MZAMIRU akiamua kukichafua, ila anapoteza sana pasi.

3. Kapombe japo maji (majaro) yake hayana faida
Mzamiru hajacheza vizuri kwa karibu mechi 10 au zaidi zilizopita za mashindano, mipira ina mgonga gonga tu. Inonga yuko vizuri ila nadhani ni namba 2 ila na yeye alikuwa nje ya uwanja kwa muda. Kapombe hajakosa mechi hata moja ya mashindano toka amerudi na mechi zote amecheza dakika 90, na kadi labda ana moja ya njano. Kumbuka tofauti na Inonga, Kapombe inabidi apande na kushuka na vyote hivyo amekuwa anavifanya kwa uwezo mkubwa sana.
 
Timu ikiwa mbovu haiwezi kuwa na mchezaji BORA.
 
Kama umefuatilia uchezaji wa Shomary Kapombe toka amepona majeraha yake amekuwa anacheza kwa kiwango kikubwa na kujituma kuliko mchezaji yoyote pale Simba.

Kama kumbukumbu zangu ziko vizuri, ni kama game moja tu ndiyo kidogo alikuwa na changamoto uwanjani.

Kama kuna mchezaji wa Simba alistahili udhamini kama ule wa CRDB basi ni Shomary Kapombe.
Shikamoo mganga.
 
Yani hili silipingi Kapombe amekuwa na muendelezo mzuri tangu atoke majeruhi, hata game na Raja jamaa alionekana Ni threat Sana ule upande wake
Hata game ya Jana jamaa alipiga kazi Sana na hashuki kiwango,siku zinavyozidi kwenda anazidi kuwa bora zaidi namuona akizidi kuwa hatari zaidi,kwa sasa Kapombe ni mchezaji bora kutokana na muendelezo wake..

Sent from my CPH2083 using JamiiForums mobile app
 
Halafu anaachwa timu ya taifa wanachukuliwa wachezaji wa Ihefu. SMH.

kapombe.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Back
Top Bottom