Short story: Kuna kitu umejifunza

Short story: Kuna kitu umejifunza

Che Kalizozele

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2008
Posts
777
Reaction score
50
Kuna bwana mmoja ambae anaishi Shinyanga,nyumba ya bwana huyu iko karibu sana na baa.Hakuna kitu halikuwa hakipendi bwana huyu kama kumkuta mtoto wake amesimama karibu na nyumbani kwao akiangalia tv iliyoonesha mambo mbalimbali pale baa.Kwa kweli bwana huyu alikuwa halipendi suala hili la mtoto wake kuangalia tv ile ya baa.Umkuta mtoto huyu mara kwa mara akiangalia tv ile japo haingii kabisa ndani ya baa kwani kwa kawaida mtoto huyu usimama mbele ya nyumba yao na kuangalia tv ile ya baa,lakini bado lilikuwa likimkera sanababa yake.
Bwana huyu alipoona amechoka kusema akamwambia mwanae,nikukuta hapa siku nyingine utanijua mie ni nani.Mtoto, mtoto tuu,siku ya siku baba kamkuta mtoto wake kasimama mbele ya nyumba yao anaangalia tv ile ile ya baa,baba akapandwa na munkali,akampa mtoto wake kipigo cha mwana ukome mpaka mtoto alilala bila ya kula huku usingizi wake ukiambatana na kwikwi za kulio.Baba kuona ile hali akajua mwanae anaweza kuumwa kwani hajawahi kumpiga kiasi kile,akaamua kwenda kulala nae.Walipoamka asubuhi mazungumzo yao yalikuwa hivi.Mtoto ndo alikuwa wakwanza kusema

Mtoto,"Shikamoo baba"

Baba,"Marahaba mwanangu"

Mtoto,"Ila baba jana uliniumiza"

Hapo baba alikosa la kujibu,ikabidi mtoto aendelee

Mtoto,"Lakini baba" hapo baba mtu ikabidi ageuke kumuangalia mwnae

Mtoto,"Kama tungelikuwa na Tv ya kwetu wala usingelinipiga na kuniumiza hivi"

Hapo baba mtu ndipo alipogundua wapi amechemsha,amini usiamini baba mtu halikuwa hana hata senti tano ndani lakini jioni alirudi na tv.
 
being a parent you must learn to love and sacrifice at the same time
 
Mhhh hii imetulia unapokuwa mzazi ni vizuri kuwa makini na maamuzi wakati mwingine vipigo kwa watoto huwa havitoi mafunzo!
 
Back
Top Bottom