Shortcut muhimu kwenye kompyuta yako

Shortcut muhimu kwenye kompyuta yako

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
𝗦𝗛𝗒π—₯𝗧𝗖𝗨𝗧 π— π—¨π—›π—œπ— π—¨ π—žπ—ͺπ—˜π—‘π—¬π—˜ π—žπ—’π— π—£π—¬π—¨π—§π—” π—¬π—”π—žπ—’

1_20241127_183028_0000.png


Leo nakuletea maujanja muhimu kwenye kompyuta yako ambayo wengi walikua hawayajui, najua unatumia kompyuta kwenye kufanya shughuli mbalimbali lakini Kuna wakati ni muhimu kutumia shortcut ili kurahisisha maisha.

Shortcut muhimu ulikua huzijui zinafanya kazi kwenye window 7 , 8, 10 , 11 na 12 πŸ‘‡

βš™οΈ WINDOW KEY+ V
Inakupa uwezo wa kufungua clipboard kwa urahisi kwenye kompyuta yenye kukupa uwezo wa kuona maandishi ya kitu chochote ulicho kopi.


βš™οΈ CTRL + SHIFT + V
Inakupa uwezo wa ku kopi kitu na kuki paste kikiwa plain Text, labda ume kopi maandishi yenye rangi unataka ku paste bila kuwa na rangi tumia hiyo shortcut.


βš™οΈ CTRL + S
hii inakupa njia rahisi ya ku save kitu kwenye kompyuta yako kwa haraka, labda ume andika kitu kwenye word, notepad unahitaji ku save tumia hii shortcut nzuri.


βš™οΈ CTRL + Z
Ikiwa unataka kufuta kitu chochote ulichokiandika unaweza tumia hiyo shortcut kukiondoa inaitwa Undo wakati CTRL + Y ni redo inakupa uwezo wa kurudisha neno ulilofuta.


βš™οΈ ALT + F4
Inakupa uwezo wa kufunga program yoyote unayoiona kwenye kioo Cha kompyuta yako ila kumbuka kutumia hii ukiwa uja save ni hatari pia unaweza tumia kuzimia kompyuta.

20-Keyboard-Shortcuts-Youre-A-Moron-for-Not-Using-2-31-screenshot-1086x611.jpg


βš™οΈ CTRL + F5
inakupa uwezo wa ku refresh page au kompyuta yako ikiwa umetumia muda mrefu na kuipa nguvu Tena. Pia unaweza tumia ALT + CTRL + ENTER kufungua program yoyote unayotaka.





Ziko nyingi ila hizo ni baadhi ongezea yako ?
 

Attachments

  • 20-Keyboard-Shortcuts-Youre-A-Moron-for-Not-Using-3-58-screenshot-1-1086x611.jpg
    20-Keyboard-Shortcuts-Youre-A-Moron-for-Not-Using-3-58-screenshot-1-1086x611.jpg
    67.7 KB · Views: 5
Back
Top Bottom