Should there be communication?

I will definitely keep distance!


100% mana nako kupenda mioyo imetofautiana.... kuna mwingine unapenda all the way... haitakiwi uthubutu kumsongelea.... But wengine kweli waweza manage...
 
Dear kwani hakuna marafiki wengine wakuwa nao mpaka yy tu jamani?


Pearl Mapenzi yanasumbua sana akili, kufikiria/kupima uzito wa mambo/level ya kupuuzia au kutopuuzia/Intensity ya mapenzi kati ya wawili/wapenzi mlo pata baadaya ya kuachana na mengine kibao ndo yanajibu na kuchangia kuweza kuelewa kua is it safe kuwasiliana au NO... Kwa upande wangu Pearl Ex wangu simsogeleii....
 
ohooo.....binadamu hatuaminiki kuna siku unaweza mkajikuta ktk mazingira ya wawili tu mkajikuta mnataka kukumbushiana ya zamani....then later una regret, kwa usalama kata mawasiliano
 
Wazungu ndio wana tabia hizi na hii inatokana na wao kuwa na uhaba wa nguvu za ngono , Mimi bana katiba yangu inasema ukaribu wa mwanamke na mwanamme rijali ni ngono tu, huyo mwanamke wenyewe atakuona b w e g e eti mnapigiana simu mnaanza kuulizana rangi za mauwa na maduka yanayouza makufuli quality halaf mnakata simu , aaaarghhhh mawasiliano na ex haikubaliki popote.
JF Emotional censor detection: hii post nimeandika nikiwa na hasira kweli.
 
Embu acha uswahili...kutokulala n mwanamke unaeongea nae hakukufanyi bw.ege!!!Mi nna hasira zaidi!
 
Embu acha uswahili...kutokulala n mwanamke unaeongea nae hakukufanyi bw.ege!!!Mi nna hasira zaidi!
tunaongelea wanaume rijali hapa, lazima uelewe. hivi unajuwa kwanini wazee wa zamani walizuia hata mzee wa kiume kumuogesha mtoto wake wa kike? hehehe
 
tunaongelea wanaume rijali hapa, lazima uelewe. hivi unajuwa kwanini wazee wa zamani walizuia hata mzee wa kiume kumuogesha mtoto wake wa kike? hehehe
Kwasababu ya mfumo dume....hivi urijali maana yake ni nini???
 
Mimi naruhusiwa kuwa na mawasiliano na Ex wangu.....
Lakini mai waifu wangu haruhusiwi kabisaaaaaa!

Sihitaji kuulizwa maswali hapa!
 
Ungeandika kichwa cha uzi kwa kiswahili ingekuwa nzuri sana na nina imani ungeeleweka tu. Inakuwa kama filamu zetu za kibongo bwana kichwa kiingereza lakini filamu ya kiswahili au na wewe ni mtunga filamu??
 

Ni kweli kabisa Pearl ni vile kila mtu anyesema yes or no anakuwa na namna ya kuutetea upande wake,Mie nimekoma sitakia mawasiliano eti ya urafiki wa kawaida
Oops No thank you
 
Ungeandika kichwa cha uzi kwa kiswahili ingekuwa nzuri sana na nina imani ungeeleweka tu. Inakuwa kama filamu zetu za kibongo bwana kichwa kiingereza lakini filamu ya kiswahili au na wewe ni mtunga filamu??

Kaka mdogo....hii tabia imezoeleka sana hapa JF........sijui kwanini watu hawapendi kukienzi kilugha cha Nyerere? Damn!
 
HAPANA, NO. ki ukweli nini kilimfanya aondoke? kilichomfanya aondoke hakiwezi kumrudisha kwako. Ebu tuwe watu wenye upeo wa kuona mbali na kuheshimu utu na roho zetu.

Yanayomsibu Kabila01, anaendekeza ujinga na mtu aliyemwacha na kufunga ndoa na mwingine. Kha! fukuzia mbali. Kama mna mtoto hapo lazima muwasiline hata kama umeolewa na mtu mwingine but with respect na kum-empower mumeo kuwa na mawasiliano na mzazi mwenzio in the sense kwamba hata akitaka kujua hali ya mwanae apige kwa mume wako.

Kwa wale wasio waaminifu watajiuliza why ufanye hiivyo? unalinda masilahi ya ndoa yako na uaminifu kwa mume wako aliyejitoa muhanga kukupenda wewe na mtoto asiyewake.
 


Bishanga wajua akili hazilingani..wewe unaweza kuamua kuwa rafiki na moyoni ukaiweka ,,kumbe mwenzio kakubali ili kukuridhisha nia yake na madhumuni akuharibie

Mungu katupa akili tofauti kwa kila mmoja.Na kwa vile katupa akili ya kujua jema na baya ukihisi hili litakuwa baya huko mbeleni ni vyema kuliepuka bado asubuhi ...Nina maana kubwa ya kusema hivi
 
Kuendeleza mawasiliano au la inategemea na sababu ambazo zilifanya muachane. mimi sioni tatizo lolote la kuwasiliana na my ex, kitu cha kuangalia tu ni kutovuka mipaka. lakini eti kakuambia mama yangu kafariki au kaka yangu anaoa na una uwezo wa kushiriki eti usiende sababu mmeachana? labda kama sielewi mawasiliano gani mnayoyazungumzia, lakini kama simu, chat, kutoka open place na kunywa bia ...... mimi kwa kusema ukweli sioni tatizo lolote hapo
 
ah ah ah kwakweli nimekuelewa kwamba fikra sahihi huja kwa lugha sahihi,ushauli copied and will be pasted soon.
Ungeandika kichwa cha uzi kwa kiswahili ingekuwa nzuri sana na nina imani ungeeleweka tu. Inakuwa kama filamu zetu za kibongo bwana kichwa kiingereza lakini filamu ya kiswahili au na wewe ni mtunga filamu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…