Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Katiba yetu ni madudu, ilitengenezwa kwa ajili ya kulinda ka kikundi cha watu. Tuanzie hapo ndio kwenye muarobaini.

Kwa sasa Rais anafanya chochote, ukihoji kuna watu watakuja kukuuliza kwani amekiuka katiba? na Je amevunja sheria yoyote? Jibu litakua hapana.

Ngoja nipitie rasimu ya warioba nione inasema nini kuhusu sifa za mtanzania kugombea ubunge, hapa pia kuna tatizo la msingi, Ikiwa bunge litapata "meno yake" ndani yake halitakiwi kuwa na wabunge wa aina ile waliopo bungeni kwa sasa.

Kwa mambo kama hayo, inahitajika nguvu ya umma ya ziada na isiyokua ya kawaida kupata katiba mpya inayotokana na rasimu ya warioba. It is almost impossible.
 
Umenena vyema.

Nakushauri P, Rudi kwenye kale ka utabiri ulomtabiria Tulia kuwa Rais ajae wa kike 2030.

Naona kama amerogwa, karukwa na akili, anatangaza vita Kwa mamlaka yepi???

Eti nyooka nao, nani alishauri viongozi wapimwe akili vile!!!!

Wana Sheria tumeaibika sana time hii!!!
 
Baada ya kunyimwa ubunge wa EA naona akili zimeanza kurudi
Mkuu with all my respect kwako, si vema to play a man,cheza mpira ambao ndio mada iliyopo, wote tumepitia challenges nyingi tu kimaisha ila bado tunapambana na maisha ,ubunge ule ulikuwa wa kupigiwa kura sio wa mtu kuteua
 
Mkuu with all my respect kwako, si vema to play a man,cheza mpira ambao ndio mada iliyopo, wote tumepitia challenges nyingi tu kimaisha ila bado tunapambana na maisha ,ubunge ule ulikuwa wa kupigiwa kura sio wa mtu kuteua
chama hakimtaki, ubunge wa kawaida kura moja, kura moja kwa mtu maarufu kama yeye ni aibu kubwa na fedheha
 
Tunafanya vip bila katiba mpya mzee
Katiba mpya inakuja, tena ni vile tuu Mungu amemuita kwake kwa ajili ya kumpangia majukumu mengine, lakini ilikuwa atuachie katiba mpya!. Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. hivyo hili sasa liko mezani kwa Mamaa!.
Nafurah umetambua kwamba nothing will change by pompering your master..
Mimi ni self employed, I don't have a master, I'm my owm master, and I have never pompared anyone!. Wanaofanya pompering ni machawa!. Mimi sio chawa!. Je, wajua Sio Kila Kumpongeza, ni Kujikomba/Kusaka Teuzi? Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
Mapendekezo haya ni mazur yakiingizwa kwenye katiba mpya
Asante tutayaingiza!.
P
 
Sasa tujibu hoja ipi ya kiingereza au kiswahili?

Chagua lugha moja na kisha jenga hoja yako,usichangie kama vile unataka kutuonyesha wewe ni nguli uliesahaulika.

Pascal Mayalla nadhani sasa ni .....
Wakati muafaka umtafute swahiba wako mzee Kikwete, umuulize ni wapi ulimkosea.na ikibidi ufanye kama Nape kwa JPM.

Maana karibu wenzio woote wameisharudishwa kulamba asali kundini ila wewe tu.

Au kuna sehemu ulikanyaga waya wake aisee!
 
Ccm mtajuana wenyewe bhana ss ambao mnatuita vibaraka wa mabeberu tunaendelea na Ibada zetu za kumuomba Mungu alipize kwa niaba yetu.....
 
Nimeelewa hoja yako ila kaka hiki kiswakinge kilikuwa na ulazima? Kwamba ungetumia kiswahili moja kwa moja usingeeleweka?..
Mkuu Asprin, jf ni social media, hivyo hakuna tatizo kuchanganya lugha, unatumia maneno you are comfortable with. Katika kusaidia kukikuza Kiswahili, naomba tafsiri ya maneno haya

Demand​

Right to Information​

Key Posts​

Endorsed​

Security of Tenure​

Oh nimesahau kumbe wewe ni mmojawapo wa "learned brothers" lazima uoneshe umahiri kwenye lugha zaidi ya moja.
Hapana, sichanganyi lugha kwasababu ya being a learned brother, nachanganya lugha just for comfort and plesure!..
Niko more comfortable kumwambia mtu maneno haya ya Kiingereza,
I love you vs nakupenda wewe
I miss you vs ?
Sorry vs samahani
Game vs ...
Etc
Tukirudi kwenye hoja... Nadhani umefika muda muafaka rasimu ya katiba ya mzee Warioba ipitishwe kuwa katiba rasmi
Naunga mkono hoja ila kwa maoni yangu, rasimu ya Warioba isipitishwe vile vile kama ilivyo, bali ifanyiwe maboresho, ikipitishwa vile vile ilivyo, tutapata bora katiba, wakati kiukweli sasa hapa tulipo Watanzania tunapaswa kupata katiba bora. Bora Katiba tuikubali, tusiichukie CCM kwa sababu CCM itahukumiwa na Karma kwa Uovu wake
Vinginevyo thread za namna hii zitaibuka kila siku. Ilipigiwa kifua na wapinzani naona hivi sasa hata Sukuma gang wanaona umuhimu wake....
Japo mimi ni Msukuma, sijawahi kuwa Sukuma Gang!. I don't believe this thing Sukuma Gang do exist in reality!. Msamiati mpya wa SUKUMA GANG haufai, unaweza kuleta matatizo kwenye jamii hapo baadaye. Mamlaka ziliangalie hili
Mwendazake angekuwa hai hivi sasa hii thread isingeanzishwa...Mungu yu mwema daina
Acha hizo, threads ngapi zimeanzishwa wakati yupo?.
P
 
Ni jambo la msingi kabisa hili.
Mawaziri wasiwe wabunge. Rais akichagua. Bunge linafanya vetting na kupiga Kura but since nchi yetu bado changa Rais apewe veto. Bunge lilikataa bado anapiga veto mradi msimamo wa Bunge anaujua.
Itawezekana ikiwa sisi wananchi tutabadikika na kuchagua wabunge watakaotuwakilisha Kwa moyo. Bunge lilivyo hivi Sasa haliwezi kufanya vetting
 
Funguka kwanini magharibi wanapinduana, walikosea wapi?
 
Hii katiba tuliyoiga wingereza itatuletea tabu, Ile ni nchi ya kifalme, katiba yao Ina mambo ya woga na waswas Kwa maslahi ya mfalme. Kwetu itatusumbua sababu sisi hatuna mfalme tuna Rais.

Athari zake ni kubwa maana inawapa mamlaka makubwa sio Rais tu, Hadi wakuu wa wilaya na wengine. Kila kiongozi katiba hii inampa kucha refu sana

Hii katiba ilitakiwa kubadilishwa tangu enzi ya mwalimu
 
Mkuu chotera , sio kweli kuwa katiba hii ya 1977, hakuna demokracia, kuna demokrasia za aina nyingi, katiba ya Tanzania, ya mwaka 1977 ilikuwa no katiba ya mfumo wa chama kimoja cha siasa, kwa sisi wa zamani tumeshuhudia uchaguzi wa kidemokrasia ya chama kimoja, watu walichuana kiukweli ukweli ila kwenye urais ndio mgombea ni mmoja anaongea na kivuli.

Tulipoingia vyama vingi ile 1992, tulipaswa tubadili katiba, tuwe na katiba ya vyama vingi, kilichofanyika ni kubadili tuu baadhi tuu ya vipengele.

Tatizo kubwa la katiba ya sasa ni ubakwaji uliofanywa kwa haki kuu ya kisiasa, zilizotolewa na katiba, kubakwa kwa kuchomekewa kiubatili (kubaka) kwa vipengele vinavyopora haki hizo.

Haki Kuu za kisiasa ni ibara ya 5, haki ya kupiga kura na Ibara ya 21 haki ya kuchaguliwa.

Haki ya kuchagua bado ipo kwa kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 yuko huru kujiandikisha kupiga kura na kuchagua kiongozi anayempenda. Hivyo haki hii ipo.

Ile haki ya kuchaguliwa sasa ndio imeporwa na shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa!. Uanachama wa chama cha siasa ni hiyari, lakini ili Mtanzania aweze kushiriki uchaguzi kugombea nafasi yoyote ya uongozi, analazimishwa lazima ajiunge na chama cha siasa, ili adhaminiwe na chama cha siasa. Shurti hilo linawanyima haki Watanzania wengine wote wasio wanachama wa vyama vya siasa.

Bila hata katiba mpya, ubakaji huu unaweza kuondolewa!.
Phttps://www.jamiiforums.com/threads/shurti-la-kudhaminiwa-na-chama-kugombea-uchaguzi-ni-shurti-batili-kwa-mujibu-wa-katiba-linatutia-hasara-tulifute.1388948/
 
Paskali, unayoyasema yatawezekanaje wakati kuna GENGE la WANAFIKI ambao kila kukicha wanasema CCM itawale milele? Yasemekana wewe ni Mshauri Mtaalam wa hilo GENGE LA WANAFIKI.
 
Inahitajika katiba mpya ambayo ni bora na sio katiba mpya ilimradi ni mpya.Ukiwa na katiba bora inayojisimamia kila kitu kitakaa kwenye mstari na atakayeharibu atakutana na makali ya msumeno wa sheria.Tatizo la afrika ni kwamba hatutaki kua na kitu kizuri kwasababu miongoni mwetu tunaishi kwa ubinafsi na ujanja ujanja.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mulamula ana elimu, akili, uzoefu, ufahamu mpana, maarifa mengi kumzidi boss wake hapo ndio shida, mwenye macho akiongozwa na kipofu lazima ajikwae au aanguke na aumie vibaya.
 
Kipindi Cha MAGUfooool ilikuwaje Kwan...tuendelee na mtiririko huo huo
As far as MAGUFULI alijaza wasukuma, Samia na yeye Ana haki ya kuteua atakavyo hata Kama ni watoto, na dada zake
 
Mawaziri wawe wanachaguliwa na wananchi na asiwe mbunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…