Show ya Werrason yakwama kutokana na kuchelewa kwa safari ya ndege ya Kenya Airways

Samwel Ngulinzira

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
1,829
Reaction score
1,972
Bila shaka wale wapenzi wa burudani hasa muziki wa Congo watakua wamekumbana na kadhia hii ya kuahirishwa kwa show ya nguli wa burudani Noel Ngiama 'Werrason"iliyokua ifanyike tarehe 6 mwezi april 2018.

Show hii iliyosubiriwa kwa hamu imeshindikana kufanyika kutokana na kuahirishwa kwa safari ya ndege ya shirika la Kenya Airways. Show hii imesogezwa mbele hadi jumamosi ya tarehe 14 mwezi april mwaka 2018.

Kuna vitu vya kujifunza kwenye kadhia hii. Kwanza suala la kuchelewesha ndege lina madhara makubwa sana, mbali na kuchelewa kufika kwa wasafiri linachafua jina la shirika husika.

kama ingekua ATCL ndo wamechelewesha safari hii wangekula madongo (matusi) hadi mkulu akapanga ratiba ya dharura ya uzinduzi ili kuzima stori.
kitu kingine cha kujifunza ni kuachana na kufanya kazi kwa mazoea, hii tabia ya kuahirisha safari imekua inajirudia sana.

Kama tunataka shirika letu likue lazima tuwe serios na kazi, mambo ya kuchelewesha safari kisa tunamsubiri kiongozi fulani inabidi tuachane nayo vinginevyo itakuja kutucost in the future.

Kwa wale waliojiandaa kwa shoo tujiandae coz Jumamosi inakaribia na wale walioko mbali na mjini wafanye kuweka MB za kutosha wakati Dar itakapokua iko busy na Werrason.

 
.....
......Noel Ngiama nzembela bango dah niko mbali sana hii Kitu ningetia timu...mwenye update skwadi line ya Weraaa atupie
 
Kuna baadhi wa watu wanasema tuwaige wa Kenya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…