Elections 2010 Show za bure zaandaliwa kuharibu kampeni za Dr Slaa

DCONSCIOUS

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Posts
1,269
Reaction score
473
Nipo nje ya jiji la dar lakini nimebahatika kupata habari kuwa kunawatu hapo dar wameandaa show za bure ili watu wakose fulsa ya kumuona na kumsikisiza Dr slaa. Kwan hali ipo wazi kabisa kuwa slaa anaugwa mkono na vijana waliowengi ambao weng wao wanapenda mziki. Kama kuna mtu ana habari zaidi atupatie taarifa.
 
watu hawadanganyiki tena, sidhani kama kuna show inayopendwa Tanzania kama English Premier League, lakini jana maeneo mengi watu waliswitch ITV kumwona Mkombozi, kwa hilo wamechemsha
 
Watanzania hawataki tena fiesta wanataka kuboresha maisha yao, na kama jana waliweza kuweka mpira pembeni na kumwangalia dr Slaa kw masaa 2, hizo fiesta hazisaidi..
 
Ni kweli naungana na hoja yako.
hapa jirani kwangu umeme ulileta matatizo na kwenye social hall pekee yenye generator kuliandaliwa free show na mshehereshaji alikuwa anajisahau na kusema ccm juuuuu!!! Ukumbi unaitwa LULU pub maeneo ya kigamboni.
show ilikuwa inakiuka sheria kwa kupiga sauti kubwa hata kuharibu usikivu kwa walio jirani. na iliisha muda mchache baada ya hotuba.

Dawa ni kuappeal kwa ITV warejeshe hicho kipindi maalumu marudio siku ya jumamosi ili kuwaweka sawa watu. hata leo jioni.
 
mkuu hata show gani iandaliwe haitajaa kabla ya mikutano ya huyu jamaa... waulize simba mwanza ilikuaje mechi ya jumatano??

utasikia na utaniambia
 
mkuu hata show gani iandaliwe haitajaa kabla ya mikutano ya huyu jamaa... waulize simba mwanza ilikuaje mechi ya jumatano??

utasikia na utaniambia
ni kwamba umeme ulikatwa na watu tulipokimbilia kwenye hizi kumbi tukakuta shows za bure zinaendelea. mie nikaamua kurejea home kufuatilia mdahalo kupitia kwa member aliyekuwa anasikiliza bongo radio.
 
watz hatudanganyiki tena jaman, mie jana nlikuwa na party ya harusi ya kaka yangu, amini usiamnini watu waliwahi sana eneo la karibu na ukumi but baa za jirani zilizokuwa zinarusha mdahalo ungedhani ndo kumbi zenyewe, harusi ilianza saa nne kasoro, hakuna watu ndani wanataka kujihakikishia je jpili iayo kura zao wanazicast kihalali au laa? kila mtu alikuali kwel tunae kiongozi mwenye vision, asieogopa kukemea! vote for Slaa and Chadema Mps next sunday
 
Sisi hapa tukisema kuwa kikwete ni bingwa wa hoax mnasema sisi ni pro chadema. haya angalia na yeye anavyoelemewa kwenye facebook page yake.
Watanzania bila uoga wanamtolea uvivu huku wakiwa hawana uoga. na wanaomtetea hawajui hata sababu ya kumtetea wanabaki kutukana tu
cheki hapo chini

Yaani ukweli ni kwamba ninastushwa sana ha huu mwamko wa watanzania. I thought ni sisi JF pekee kumbe kuna wanaharakati kila kona wanamweka kwenye kona mheshimiwa.
Naamini anazisomaga hizi hoja ndo maana ataitisha mkutano hiyo ijumaa o jumapili
 
Hahahahahah!! watu wamechoka haki yanani. Jamaa wamemwaga laivu bila kuogopa ni kama Madr Slaa wotee. Good movie!
 
wana jf hatutakiwi kukata tamaa pls vote for slaa mimi naamini kama mungu amepanga mafisadi hawawezi kupangua
 
Wana JF mimi nilikuwa Bukoba 14/10/2010 Dr alikuwa na mkutano mkubwa sana (nilihudhuria) hapo kwenye uwanja wa Mashujaa, kwa siku hiyo hiyo ccm waliandaa tamasha la mwalimu kwa kupiga muziki wa bure kwenye uwanja wa Kaitaba. waliambulia watoto tu, hata walipotaka kutoka gate la uwanja lilifungwa wakubwa waliruka ukuta watoto wakabaki hadi mku5 wa Dr Slaa ulipokwisha. Kwa mara ya kwanza sisiem wanamwenzi Mwalimu kwa disco!!!!!!!!!!!!!
 
iko siku tutanza kuwa susia na wasanii wanao tumika...nimependa avatar yako
 
dr slaa tosha! hatudanganyiki 2010! ni aibu kwa kijana mtanzania kudanganyika!
 
ccm is just another substitute for a paper that u use comfortably when taking two aka pop!
 
hahahaahahaaaaaaaaa yaani wanamchakachua live hadi kwenye facebook yake
yaani wewe tembelea kule kwenye book yake uone wanavyomzabua rais wima wima.
sisi tupo hapa tunapaswa kupeleka hoja zetu kule pia maana inaonesha wapo wanaompelekea nin kimepostiwa.
ila caution kule hakuna pen name.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…