Kanal Hilal
Member
- Feb 4, 2017
- 62
- 121
Kuna matukio mengi sana hutokea kwenye jamii na wanajamii huyachukulia poa. Na pengine baadhi ya hayo matukio umekuwa ukiyashuhudia kwa macho au umekuwa ukiyatenda kila kukicha pasi na kutambua kuwa hayo ni miongoni mwa matukio ya ya Ukatili wa Kijinsia. Ni wazi kuwa tulio wengi hatujui maana halisi ya Ukatili wa Kijinsia.
Ukweli ni kwamba Ukatili wa Kijinsia ni somo kubwa na lenye uwanja mpana sana. Kwenye jamii tunayoishi mimi na wewe matukio yatokanayo na UKATILI WA KIJINSIA yamekithiri sana kuliko vile tunavyodhani.
UKATILI WA KIJINSIA NI NINI???!!!
Ni tendo lolote lile analofanyiwa mtu yeyote pasi na hiari yake, tendo hilo aidha muathiriwa atafanyiwa kutokana na udhaifu wa jinsia yake au umri wake. Mara nyingine matendo hayo hufanyiwa mtu mwenye matatizo ya akili (mwendawazimu) au yule wenye matatizo ya mwili (mlemavu).
Matendo ya Ukatili wa Kijinsia yapo ya aina mbali mbali na anaweza kufanyiwa mwanamke au hata mwanaume, mtu mzima au hata mtoto.
UKATILI WA KIJINISIA NDANI YA NDOA.
Mwanamke ambaye yupo kwenye ndoa au ainaishi tu na mwanaume ambaye ni mpenzi wake (hawara). Mwanaume amekuwa akirejea nyumbani usiku wa manane kila siku tena amelewa njjjwwiiiii. Na akifika tu nyumbani anamlazimisha huyo mwanamke kufanya tendo la ndoa (sex), hata kama mwanamke atakuwa hajisikii na hayupo tayari kwa tendo hilo. Mwanamke anakataa kata kata lakini mwanaume anamlamisha na tena anatumia nguvu hadi kufanikisha lengo lake. Kuna wakati anamuingilia hadi kinyume na maumbile. Mwanamke amekuwa akiishi na jambo hilo huku akiumia sana moyoni. Na hamuelezi mtu yeyote kwa kuhofia kuharibu uhusiano wao na aibu huku akijiambia "nikiliweka hadharani watu watanichukuliaje??!!". Hilo ni moja kati ya matukio ya Ukatili wa Kijinsia.
UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO.
Kuna mtoto wa kiume au wa kike. Analala chumba kimoja na binti wa kazi au kijana ambaye yupo hapo nyumbani, awe rafiki, jamaa au hata ndugu wa damu kabisa. Kila siku usiku huyo mtoto anaingiliwa kimwili (kubakwa) na mtu huyo huku akitishiwa kudhuriwa endapo atatoa taarifa hizo nje. Na kama ilivyo kwa watoto, ni waoga kwahiyo anaishi na hilo tatizo moyoni huku akipata athari kubwa sana za kiafya na kisaikolojia. Huo ni Ukatili wa Kijinsia.
UKATILI WA KIJINSIA NYUMBANI KWAKO.
Kuna binti wa kazi anayewasaidia shughuli za kazi hapo nyumbani. Kila ukitoka mume wako, kaka yako, mwanao wa kiume au hata baba yako mzazi anamlazimisha kufanya ngono bila hiari yake huku akimtishia kumfukuzisha kazi kama atasema jambo hilo. Huo ni Ukatili wa Kijinsia.
UKATILI WA KIJINSIA OFISINI.
Mke wako anafanya kazi katika kampuni au ofisi fulani. Bosi wake anamtaka kingono na anatumia cheo chake cha ubosi kutimiza azma yake. Mkeo haridhishwi na jambo hilo lakini atafanyaje??!! Akikataa tu anafukuzwa kazi. Ingawa tendo hilo linamuumiza, na hana namna nyingine ya kufanya zaidi ya kukubaliana na matakwa ya bosi wake ili kulinda kibarua chake. Huo ni Ukatili wa Kijinsia.
UKATILI WA KIJINSIA SHULENI/VYUONI.
Mtoto wako, awe binti au kijana wa kiume. Kuna mwalimu anamuingilia kimwili (kumbaka) huku akitishia kumuadhibu au hata kumfukiza shule/chuoni. Tendo hilo linamuumiza sana lakini hawezi kusema kutokana na kuhofia adhabu na aibu. Na hii imekithiri sana kwa vijana wa kiume kuingiliwa (kulawitiwa) na walimu wa kiume. Huo ni Ukatili wa Kijinsia.
Inaumiza sana.
Kama nilivyosema hapo awali, matukio haya ya UKATILI WA KIJINSIA yapo mengi sana na yanafanyika kila siku. Yanafanyika mashuleni, vyuoni, ofisini, kwenye kwaya za kanisani na madrasa za masomo ya kiuslamu. Na hapo nimeongelea katika upande wa ubakaji tu, sijagusa kabisa ukeketeji wa mabinti na upande wa adhabu kama vile vipigo na adhabu zinazotweza utu wa mtu.
Kwa upande wa vipigo ndio usiseme. Wanaume wengi tunawapiga wapenzi wetu pindi tunapohisi wametukosea. Bila kujua kuwa katika hilo nasi tunashiriki katika kufanya matendo ya Ukatili wa Kijinsia.
NINI KIFANYIKE KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA??!!.
Sisi kama jamii tunapaswa kupiga vita Ukatili wa Kijinsia katika kila nyanja. Na tena tupige vita kwa nguvu zetu zote. Tunapaswa kulipokea jambo hili kama JANGA LA TAIFA. Na pengine ni janga la dunia maana Ukatili wa Kijinsia upo katika kila pembe ya dunia. Sisi kama jamii tunapaswa kuandaa agenda maalumu ya kupambana na tatizo hili. Na serikali pamoja na wadau mbalimbali wahakikisha wanatoa elimu kwa jamii juu ya kuacha kuwanyanyapaa wale walioathiriwa na matukio hayo ili wawe tayari kutoa taarifa za ukatili pindi tu wanapotendewa.
Na Hilal Kanal
0718022322
#UkatiliWaKijinsia
#Ubakaji
#Ukeketaji
#Serikali
#Jamii

Upvote
1