Wivu si kitu kibaya katika mapenzi. Huonyesha mapenzi aliyonayo mtu, ingawa ikizidi ni tatizo kubwa. La msingi ni kumshauri na kumuonyesha kuwa wewe ni mtu ambaye unajiamini na unamuamini mpenzio na kamwe si mtu wa kudandia wanawake hovyo.
Inawezekana huo umri wake ndiyo unamfanya ahisi kwamba unaweza kuwa na vimwana nje. Muonyeshe upendo na ukaribu na msisitizie mara kwa mara kuwa umeamua kuwa naye yeye tu na unampenda kwa dhati regardless ya tofauti ya kiumri.
Suala la kuacha mishe mishe zako na kwenda kusimamia miradi yake kwangu halina msingi maana kama una tabia mbaya unaweza kuiendeleza hata hapo kwenye miradi yake na pia naona kama si picha nzr sana kwa mwanaume kusimamia miradi ya mpenzio wakati hata ndoa naye bado! Unaweza usieleweke!
By the way, kwa nini unahangaika na shugamami wakati mabinti wa umri wako wapo wengi? Je, ni kwa ajili ya hivyo visenti na miradi yake? Kama ndvyo aisee, wewe ni mwanaume, badili tabia na jitafutie kwa jasho lako.