Shughuli za Kibinadamu zinaharibu Mazingira na kuweka hatarini Mustakabali wa Maisha ya Vizazi vijavyo

Shughuli za Kibinadamu zinaharibu Mazingira na kuweka hatarini Mustakabali wa Maisha ya Vizazi vijavyo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Shughuli za kibinadamu zimepelekea uharibifu mkubwa wa misitu na ukataji Miti kwa ajili ya kuni na mkaa ambao unaweka hatari kubwa kwa vizazi vijavyo.

Uharibifu huu wa misitu una athari kubwa kwa mazingira na ustawi wa binadamu.

IMG_7344.jpeg

Misitu ina jukumu kubwa na muhimu katika kudhibiti mzunguko wa maji. Hufanya kama mabwawa ya asili kwa kusambaza na kuhifadhi maji ya mvua.

Kufyeka maeneo makubwa ya misitu kunavuruga uwiano huu nyeti na kusababisha upungufu wa maji na hatari zaidi ya ukame na uhaba wa maji. Pia inapelekea maji kuongezeka baharini. Mfano, madhara makubwa kabisa tunayaona Ziwa Victoria maji yameongezeka, hii inaashiria kabisa kuwa watu wamekata miti maeneo ya Basin ya ziwa Victoria.

Kupoteza misitu pia kunachangia mmomonyoko wa udongo, kwani mizizi ya miti husaidia kushikilia udongo na kuzuia mmomonyoko unaosababishwa na mvua kubwa.

Ili kulinda mustakabali wa Misitu na Mzingira, hatua za dharura zinahitajika. Serikali, mashirika, na watu binafsi wanapaswa kuzipa kipaumbele jitihada za kupanda miti na kuitunza katika maeneo yaliyoathiriwa na uharibifu wa misitu.

Njia endelevu za usimamizi wa ardhi zinapaswa kutekelezwa, kama vile kilimo shirikishi na upandaji tena miti kwenye ardhi iliyoharibiwa ili kurejesha ikolojia ya misitu.
 
Hii ndiyo shughuli hasa ya NEMC wanayotakiwa kuifanya kupambana na uharibifu wa mazingira, sio kukimbila kupambana na kelele za shangwe na raha kwenye mabaa na kelele za ibada ambazo kimsingi si kelele hasa
 
Write your reply...MKOA WA TANGA NA PWANI MISITU IMEISHA
 
Back
Top Bottom