Aina yoyote ya uwepo wa binadamu ndani ya hifadhi lazima ina athari zikiwemo uchafuzi wa mazingira pamoja na usumbufu kwenye mfumo wa ki ikolojia... swala ni kiwango cha athari hizo na namna ambavyo tunasafisha au kuzipunguza.
Kumbuka viumbe pori siyo domestic na hawakuumbwa kuishi na binadamu kama ilivyo kwa mbwa au paka, uwepo wetu sisi pekee ni changamoto. Simba akimzoea binadamu au akizoea magari tayari ni badiliko kwenye tabia yake ya asili. zaidi ya hivyo kelele, moshi wa magari, kutupa chupa na mabaki ya vyakula na mambo kama hayo huongeza kiwango cha uchafuzi/usumbufu.