Shuhuda: Kutoka Kuwa Muosha vioo vya magari kwenye Mataa sasa kwenda Kumiliki Biashara

JOHNGERVAS

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
1,011
Reaction score
1,681
Kuna Video inasambaa kwenye Mitandao ya Kijamii nikaona niwashirikishe kuna la Kujifunza

=============

Victor Tesha

Nilikutana na mvulana mdogo sana ambaye kila siku alikuwa akisafisha kioo cha mbele cha gari langu kila niliposimama kwenye taa za trafiki hapo Moroco. Niliona jitihada zake na uvumilivu wake, nilikumbuka nilipotoka na nikahisi deni la kumsaidia. Jana, nilimwalika ofisini kwetu. Alisafisha ofisi na alikuwa na furaha sana. Wiki ijayo tutamfungulia biashara kwa ajili yake. Na tutamfundisha namna ya kukuza biashara yake. Ana nidhamu na hatumii madawa ya kulevya wala hanywi pombe.

Tunashiriki kitendo hiki cha wema ili kuwahamasisha kila mtu afanye mema na kugusa angalau maisha ya mtu mmoja. Hebu tufanye dunia yetu na Tanzania kuwa mahali pazuri pa kuishi.

Kuwa mwema, si kwa wengine tu, bali pia kwako mwenyewe. Dunia ni ngumu vya kutosha bila kuongeza uzito zaidi. Onyesha wema katika maneno yako, matendo yako, na mawazo yako. Haitaji mengi—tabasamu, sikio la kusikiliza, au uvumilivu wa muda mfupi. Wema una njia ya kusambaa, kugusa maisha kwa njia usizoweza kufikiria. Unaunda miunganisho, uponya majeraha, na kuleta nuru mahali penye giza. Katika dunia inayoweza kuwa baridi na isiyojali, kuwa joto. Kuwa mwema, kwa sababu kila mtu anapambana na vita usivyojua.

Tayari huu sio msaada tena. Angalau basi hata ungepiga kimya hadi pale atakapoanza biashara yake. Tabia ya kujionyesha kuwa wewe ni mwema ni ujinga mtupu.
Anaonyesha ili watu wajifunze hiyo sio sadaka mkuu ni msaada.
 
Acha hizo mkuu
Mkubwa mimi ni mtu mzima na akili yangu, ukitaka kuamini hilo,nipe full info za huyo jamaa na ofisi yake nikuletee taarifa zake. I am sure jamaa ana matatizo. Morocco na waosha magari serious. Na wewe unaamini.
 
Hakuna kitu hapo zaidi ya upuuzi mtupu. Ukimsaidia mtu lazima uchukue video?
Hiyo video imekuathiri kwa namna yoyote/ Je ina Impact gani ka jamii? Watu wangapi wataiona na kubadili zile dhana wanazoamini vijana hao ni wahuni, vibaka na wezi?
 
Mkubwa mimi ni mtu mzima na akili yangu, ukitaka kuamini hilo,nipe full info za huyo jamaa na ofisi yake nikuletee taarifa zake. I am sure jamaa ana matatizo. Morocco na waosha magari serious. Na wewe unaamini.
Mfuate huko instagram anaitwa Victor Tesha
 
Kuna Video inasambaa kwenye Mitandao ya Kijamii nikaona niwashirikishe kuna la Kujifunza

=============

Victor Tesha

Nilikutana na mvulana mdogo sana ambaye kila siku alikuwa akisafisha kioo cha mbele cha gari langu kila niliposimama kwenye taa za trafiki hapo Moroco. Niliona jitihada zake na uvumilivu wake, nilikumbuka nilipotoka na nikahisi deni la kumsaidia. Jana, nilimwalika ofisini kwetu. Alisafisha ofisi na alikuwa na furaha sana. Wiki ijayo tutamfungulia biashara kwa ajili yake. Na tutamfundisha namna ya kukuza biashara yake. Ana nidhamu na hatumii madawa ya kulevya wala hanywi pombe.

Tunashiriki kitendo hiki cha wema ili kuwahamasisha kila mtu afanye mema na kugusa angalau maisha ya mtu mmoja. Hebu tufanye dunia yetu na Tanzania kuwa mahali pazuri pa kuishi.

Kuwa mwema, si kwa wengine tu, bali pia kwako mwenyewe. Dunia ni ngumu vya kutosha bila kuongeza uzito zaidi. Onyesha wema katika maneno yako, matendo yako, na mawazo yako. Haitaji mengi—tabasamu, sikio la kusikiliza, au uvumilivu wa muda mfupi. Wema una njia ya kusambaa, kugusa maisha kwa njia usizoweza kufikiria. Unaunda miunganisho, uponya majeraha, na kuleta nuru mahali penye giza. Katika dunia inayoweza kuwa baridi na isiyojali, kuwa joto. Kuwa mwema, kwa sababu kila mtu anapambana na vita usivyojua.

View attachment 3055962
Sawa
 
Ni jambo jema ila kijana pia asibadilike tabia tu baada ya kuanza kuingiza hela nyingi,aendelee na hiyo hiyo nidhamu yake na kujituma ili atimize ndoto zake,

All the best young Boy.
 
Umejitokeza mapema mno kutangaza huo msaada , ungesubiri basi hata msaada wenyewe uzae matunda ndio ushuhudie vizuri zaidi, pengine hata yeye aliyesaidiwa angewashudia watu
 
Mtu anapotoa msaada wake ndiye anayeamua na anajua lengo la kufanya hivyo maana wanaweza kujitokeza wengine na kushauri zaidi nini kifanyike. lakini mwisho wa siku yeye anajua kwa nini amepost
 
Back
Top Bottom