Shuhuda za mikasa mbalimbali michezoni

Shuhuda za mikasa mbalimbali michezoni

qarem

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2018
Posts
626
Reaction score
825
Hi wana JF

Twende moja kwa moja katika mada,lengo LA Uzi huu ni kuhadithiana mikasa mbalimbali tuliopata wakati wa michezo mbalimbali.

Binafsi ni mpenzi wa mpira wa miguu,nishawahi kupata mikasa/AJALI za hapa na pale ila sijawahi kukoma kucheza Mpira mpaka pale umri ulipoanza kupambana na majukumu ya hapa na pale ya kimaisha hapo ndo ukawa ukomo wa kucheza mpira ila mpaka sasa bado natamani tena kuingia uwanjani lengo kuu ni kwajili ya afya na kuburudika pia.

Mikasa mingi niliipata kipindi nacheza chandimu,unaweza ukang'oka kucha,ukajikwaa na kutoa ngozi katika vidole baada ya hapo unachukua zako litambala unafunga katika kidonda na mchezo unaendelea.

Mkasa mkubwa niliopata wakati nacheza chandimu ni kuvunjika mkono wangu wa kushoto tukio lile sitalisahau,nilikua winga teleza mmoja hatari sana,basi bwana siku moja nikataka kupiga tikitaka ili nifunge goli la kideo [emoji16] kilichonikuta hata sielewi mpaka sasa, beki kisiki alikuja akanikanyaga mkono, weeee [emoji848][emoji848] niliona kizunguzungu, nyota nyota, aiseh sijui niseme nini nilichokua nakihisi mana mkono sehemu ulipokanyagwa palikua kama kuna shimo na kiganja kilikua kimekua kama kinaning'inia na ndo ukawa mwisho wa mchezo , cha ajabu wapuuzi wakanipa majani ya minyonyo kwenda kujikanda nyumbani [emoji23][emoji23][emoji23],kipindi narudi zangu magetoni bi mkubwa akaniona akaanza kuwaka, umefanya nini wewe mtoto, sikutaka kumwambia alichokuja kukiona mungu wangu alishiwa pozi [emoji856] lakin akawa ananifokea maana alikua hapendi kabisa mimi na wadogo zangu kucheza mpira mana alikua akijua hauna mana kwa kipindi hicho,sasa mfano mzuri akanipa akasema umeona umevunjika mkono kuna ambae kahangaika kukupeleka hospitali,au hata kukusindikiza kuja hapa nyumbani?? Jibu likawa hapana huku nalia.

Kwa hasira alikua kakinga maji katika bomba akanambia nikabebe tena kwa mkono ule ule nilihisi duniani nipo mwenyewe na nasulubiwa,niliacha ile kazi mara moja kilio ndo kikawa kimefunguliwa zaidi na zaidi,mwisho wa siku nikapata matibabu nikapona ila mpaka leo baridi ikizid nahisi maumivu.

MKASA MWINGINE ENZI NAPIGA GOZI LA NG'OMBE.
Hili ni moja ya tukio ambalo nalikumbuka sana mana alimanusura niwe chongo kipindi nipo advance,[emoji26][emoji44]nilivyokua mpumbavu kitu nilikua nawaza baada ya kupata ajali ilikua ni majuto ya kuwa sitakuja tena kupendwa na watoto wazuri [emoji855][emoji855][emoji855] mana kidogo nilikua nasumbuliwa sana na watoto wazur mana kasura kalikua baby face!!

Ilikua hivi, mimi nilikua nacheza kama namba kumi,basi bwana golikipa wetu alipiga mpira mbele tukashambulie mwisho wa siku tupate matokeo,ila haikua hivyo kipindi mpira bado haujatua chini mimi nikawa nakimbia ili niende nikutane nao nianze kuchanja mbuga,sasa kipindi naufuta mpira macho yote yalikua angani kuangalia jinsi mpira utakapotua na kukontro huku naelekea goli la adui yetu,

Ghafla picha la kutisha likaanzia hapo [emoji53][emoji53] beki wa timu pinzani alikua anakuja kuokoa mpira hivyo hakusubiri mpira upoe akaunga naona akaubutua ili urudi golini kwetu,ile anaubutua tu mimi nikatutana nao wa jicho la kushoto aiseeh nilipiga ukelele mmoja mpaka chini,nikajua nakata roho,nikagala gala pale chini nafumbua macho hivi jicho moja linaona kawaida lingine naona wekundu tu,nikawa siamini ninachokiona nikawa nafikicha kuona vizur aaaaah wapi [emoji53][emoji53] machozi haya hapaa aiseh [emoji22] jicho langu likawa limefunikwa na damu,likawa jekundu zaidi ya nyanya,wenzangu wakanibeba wakanisafisha na maji nikaenda kulala ila nilikua naona kwa jicho moja,mpaka nilioenda hospitali na kupata matibabu mpaka sasa nipo vizuri.

Hayo ni matukio makubwa ambayo nahisi nimeyapata kipindi hicho,na ambayo nayaona ni makubwa yapo mengi ila naishia hapo ili nisiwachoshe.

Uzi tayari karibuni wadau,mtoe shuhuda za mikasa mliokumbana nayo michezoni!!

NB; samahanini kwa uandishi mbovu!
 
Picha ni muhimu
Screenshot_20200607-203841.jpg
Screenshot_20200607-203758.jpg
 
Back
Top Bottom