Shuhudia Aibu Nyingine Ya Mwaka Na Iliyotukuka Haswa Kwa Wana Yanga

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yanga Wameweka Rekodi Nyingine Kwa Kuahirisha Sherehe Za Miaka 80 Za Yanga Na Za Miaka 25 Ya Ubingwa. Zifuatazo Ni Sababu Zenyewe Na Naomba Mzisome au Mzipitie Kisha Mtanijibia Maswali Yangu Ya Kimantiki Yatakayofuata.


  1. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Sasa Ni Mwezi Mtukufu Wa Ramadhan.
  2. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Viongozi Wa Dini Wamezizuia Kwa Sababu Zao ( Hakuzitaja ).
  3. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Wachezaji Wa Yanga Hawatakuwepo.
  4. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Timu Ya Taifa Itakuwa Ugenini Inacheza Mchezo Wake Muhimu.
  5. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Helicopter Iliyokuwa Itumike Imegoma Kutua Ardhini Kwa Siku Ya 3 Sasa.
  6. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Viongozi Wakuu Wa Simba Hawajathibitisha Ushiriki Wao.
  7. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Bado Hawajatimiza Adhma Yao Ya Kurudisha Zile Goli 5 -0 Walizofungwa.
  8. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Watu Wa Hali Ya Hewa TMA Hawajawajibu Kama Mvua Itanyesha au La.
  9. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Rais Kikwete Ratiba Zake Bado Zinawachanganya.
  10. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Imebidi Waomboleze Kwanza Hamis Kiiza Kutua Kwa " Mnyama ".Simba.
  11. Sherehe Zimehairishwa Kwakuwa Bado Wanaendelea Kunyonya Maji Ya Mafuriko Yaliyotuama Klabuni.

Baada Ya Kuziona Hizo Sababu Hapo Juu Naomba Tu Kuuliza Hivi Viongozi Wote Wakuu Wa Yanga Na Kamati Nzima Ya Maandalizi Ya Sherehe Hizo Hizo Sababu Zote Hawakuziona Muda Wote Wa Wiki 3 Zao Zilizopita Za Maandalizi Yao? Na Kwanini Msemaji Wao Jerry Muro Amekubali Kubebeshwa Mzigo Wa Kujiaibisha Tena Leo Mbele Ya Waandishi Wa Habari Kwa Kutoa Sababu Hizo 11 Ambazo Hazina " Mantiki " Na Zinazoitia Aibu Klabu Inayojiita Ya " Kimataifa? ".

Naombeni Maoni Yenu Na Naomba Kuwasilisha.
 
Acha upoyoyo wewe, thread zako hazina mantiki yoyote katika jamii. Hatuna muda wa kuchangia thread za kitoto kama hizi zako.
 
Afadhali nawe umeliona hili. Huyu jamaa toka jana anamuandama Jerry Muro, alipitiwa naye na kubwagwa nini?
 
Acha upoyoyo wewe, thread zako hazina mantiki yoyote katika jamii. Hatuna muda wa kuchangia thread za kitoto kama hizi zako.

Umesema Huchangii Sasa Hapa Umefanya Nini? Akhsante Na Wewe Kwa Kututhibitishia " UPOPOMA " Wako. Ungekaa Kimya Ingependeza Zaidi.
 
Afadhali nawe umeliona hili. Huyu jamaa toka jana anamuandama Jerry Muro, alipitiwa naye na kubwagwa nini?

Siku Zote Tanzania Mtu Mkweli Na Mweledi Huwa Hakubaliki Na " Wajinga " Na " Wapumbavu " Kadhaa ILA Kwa Mwenyezi Mungu ANAKUBALIKA!
 
Gentamicine nilikua nakuheshimu sana kwanza kama binadamu pili kama mwanahabari mahiri lakini kwa hili ni dhahir kwamba umepayuka kifikra na umefilisika kimawazo.
Wewe umekua kama supaki wa bunge na kamati ya nidhamu ya kutoa hukumu bila kumsikiliza msemakweli.

Hiyo kauli yako ya wazee wa mafuriko siitaki, tafadhali ifute isije ikaingia kwenye hansad.
 
Ushindi wa YANGA, sherehe za Yanga wewe kinakuuma nini ? au kwasababu tulichukua ubingwa katikati ya LIGI ? na msimu ujao wembe ni ule ule.
 
Yanga inakukereketa sana aisee. Ngoja nikupe dokezo, unatia aibu.
 
Mkuu GENTAMYCINE mbona hi thread yako ni dhahifu sana?
Sidhani kama kuna mwana SIMBA FC ata comment hapa kwa kukuunga mkono,maana naye pia ataonekana dhaifu kama uchumi wa tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Kumbe 5-0 bado inawaumiza vichwa mpaka mnaona aibu kuandaa sherehe
 
Mleta mada ana hoja japo huwa anazidisha chumvi sana kwenye utani wake na Yanga kiasi anajikuta anajipiga chenga mwenyewe.

Kwa masikio yangu mwenyewe nimesikia Yanga wameahirisha kwa sababu kuanzia ya 1-4! Na hapa kwa kweli mleta mada ana hoja inayohitaji kujadiliwa kwa sababu hizi sababu zilijulikana muda mrefu tu uliopita.

Wapangaji walipaswa kuzingatia haya kabla. Kuahirishwa sherehe sio issue lkn sio kwa sababu hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…