Shukrani: Baada ya kujikata na wembe wa muathirika wa VVU nimepima na kukutwa 'negative'

Nilikaa miaka saba kabla ya kwenda kupima tena HIV baada ya kumuhudumia mgonjwa wa UKIMWI wakati anajisaidia haja ndogo mkojo wake ukaingia kwenye kidonda changu ambacho kilikuwa kibichi kabisa.

Lakini nashukuru Mungu mwaka jana baada ya kuteseka sana kwa maradhi ikabidi nikapime tu kwa sababu nilikuwa nakonda bila kujua nini hasa kinanisumbua.

Ila hakuna kitu kigumu kama kusubiria majibu ya vipimo vya HIV yaani nilikuwa natetemeka kama nipo kwenye jokofu vile.
 
Hongera mkuu. Ashukuriwe MUNGU wa mbinguni
 
Jana mwenzio nilizimia tena pale doctor anavyopita mbele yang ananiangalia anarud ndan niliangua kilio nikasema tayar ninao mbona siitwi labda wanatafuta mbinu ya kuniambia
 
Sawa kama uliamua kuokoka kwasababu ya hofu uliokuwa nayo endelea kubaki hivyo hivyo,usiache kisa umesalimika maana ukiacha tu utaingizwa kwenye jaribu lingine...
 
Mkuu ulikumbuka kupima na uzito?
Maana daah kwa hio miezi 5 ya msongo wa mawazo utakua umepunguza kilo za kutosha.
Acha tu nilikuwa na kl 60 mwanzo Jana nmepma nmekuta kl 52
 
Poole my ila siku nyingine ukitaka kwenda kupima nipitie nikusindize.
 
ni kipindi kugumu sana hiki.. kusubiri majibu ni kitu kingine haswa
 
Ulikaa dk 2 ndomana nilikuwa nachanganyikiwa ila Leo nilivyongea na doctor kaniambia virus vinakaa nje ya damu kwa sekunde 5 tu
Huyo Dr wako muongo katika vijidudu vinavyostahimili hali nje ya eneo lake la kawaida ni viruses aisee ,ili kujihakikishia HIV vimekufa kabisa ndani ya bleaching agent (Chlorine 0.5%)lzm chombo kilichogusa damu au majimaji ya mwili kikae humo jumla dakika 30! We achana na hizo story zisizo na research, shukuru Mungu uko clean labda kwa kifupi mwili wa binadamu sio kwamba haupambani kabisa na HIV hapana, ukipata dose ndogo mwili unaweza ukavi eliminate vyote na hasa kama itakuwa pia uliwahi na PEP!
 
Sikutumia pep
 
Vipi ile chanjo yetu ya Ukimwi, aliyeisha ambukizwa anaweza kuitumia ?
Au ni kwa wasioambikizwa tu. Sijapata maelezo yake kwa kina.
 
Watu wanaogopa HIV huku ngono mnafanya tena peku peku.Hahahaaa
 
Vipi ile chanjo yetu ya Ukimwi, aliyeisha ambukizwa anaweza kuitumia ?
Au ni kwa wasioambikizwa tu. Sijapata maelezo yake kwa kina.
Ile chanjo ni kwajili ya watu ambao bado hawajaambukizwa ili wasipate ila kwa aliyepata ugonjwa tayar hawez kutumia Dawa ya ambaye ameshapata iko njian ndan ya miaka 5 ijayo itapatkana
 
kapime tena after 3 month, uoga wako kiboko.
 
kapime tena after 3 month, uoga wako kiboko.
Nmeambiwa haya ndo majbu ya Mwisho coz nimepima na kipmo cha UNGOLD na nina miez 5 toka nijikate ingekuwa sijafkisha hata miez 3 hapo ndoningerud
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…