kaka nimekupata embu nipe jinsi ya kuapply
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.
1. KARANI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:-
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu;
b) Kuhesabu watu kwa kutumia
dodoso fupi katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu;
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama; na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema;
b) Awe amehitimu angalau kidato cha nne;
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika,
AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika,
AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
2. KARANI MWANDAMIZI WA SENSA
Kazi za Kufanya
Mwombaji wa nafasi hii, endapo atachaguliwa atapangwa katika eneo analofanyia kazi au eneo analoishi na atakuwa na kazi zifuatazo:- 2
a) Kuhudhuria mafunzo ya kuhesabu watu,
b) Kuhesabu watu kwa kutumia
dodoso refu katika Eneo la Kuhesabia Watu na kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu,
c) Kutunza vifaa vyote na nyaraka za Sensa katika hali ya usafi na usalama, na
d) Kufanya kazi nyingine zinazohusiana na Sensa atakazopangiwa na Kiongozi wake.
Sifa za Mwombaji
Mwombaji wa nafasi hii anatakiwa awe na sifa zifuatazo:-
a) Awe na umri usiozidi miaka 60 na mwenye afya njema,
b) Awe amehitimu angalau kidato cha sita,
c) Awe ni Mkaguzi au Mratibu wa Elimu, Mwalimu katika Chuo cha Ualimu, Shule ya Sekondari au Shule ya Msingi (Shule za Serikali au Binafsi) katika eneo husika,
AU
d) Awe ni mfanyakazi yeyote wa umma anayeishi au kufanya kazi katika eneo husika,
AU
e) Kijana aliyehitimu masomo yake na hajapata ajira, na
f) Asiwe na kesi yoyote ya jinai.
3. Namna ya Kutuma Maombi
Mtanzania mwenye sifa zilizotajwa hapo juu atume maombi yake kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya/Halmashauri kwa anuani iliyowekwa hapa chini, akiambatisha nakala za vyeti na nyaraka muhimu ili kuonyesha sifa alizonazo.
Maombi hayo yatumwe kwa kujaza Fomu Maalum ya maombi ya kazi ambayo inapatikana katika Ofisi ya Mratibu wa Sensa wa Wilaya/Halmashauri, na endapo fomu haikupatikana, mwombaji atume maombi kwa kuandika barua akionyesha anuani kamili ya mahali anapofanyia kazi na namba ya simu kama anayo.
Maombi yapitishwe kwa wakuu wa kazi kwa walioajiriwa au Watendaji wa Mtaa/Kijiji kwa wale wasiokuwa na ajira, ili maombi hayo yafike wilayani kabla ya tarehe 25 Julai, 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sensa ya Wilaya
Wilaya ya
..
S.L.P
.
OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU
[TABLE="align: left"]
[TR]
[TD="width: 524"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[TD="width: 164, bgcolor: white"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MWENYEKITI WA SENSA (W)
WILAYA/HALMASHAURI YA
.
.
..
..
YAH: MAOMBI YA KUFANYA KAZI YA MUDA KAMA KARANI WA SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA YA MWAKA 2012
SEHEMU YA I: TAARIFA BINAFSI ZA MWOMBAJI (Ijazwe na Mwombaji Mwenyewe)
1.
Jina kamili (majina matatu):................................... .......................................................................
2. (a) Kazi ya sasa
(b) Namba ya Simu
3. (a) Kiwango cha Elimu
.. (b) Tarehe ya Kuajiriwa
4. Mahali (Kijiji/Mtaa*) unapofanyia kazi (Kama una ajira)
..
5. Anuani kamili ya mahali unapofanya kazi: (Kama siyo mwajiriwa andika anuani ya mahali unapoishi )
.
6. (a) Mwaka wa kuzaliwa: .....................
.(b) Wilaya uliyozaliwa
7. Jina, Anuani Kamili na Simu ya Mdhamini wako
.
8. OMBI:
Ninaomba kufanya kazi ya muda kama KARANI /KARANI MWANDAMIZI* wa Sensa ya Watu na Makazi, 2012 na ninaahidi kuwa nitatimiza masharti na maelekezo yote yatakayotolewa na Serikali ili kufanikisha kazi hii. Sahihi ya Mwombaji
. Tarehe
SEHEMU YA IIA:UTHIBITISHO KWA WALIO NA AJIRA(Ijazwe na Mkuu wa Sehemu ya Kazi)
9.
Ninathibitisha kuwa mtajwa hapo juu ambaye cheo chake ni
anafanya kazi katika kituo cha
.... na ni mkazi wa Kijiji/Mtaa*
.
.. Kata ya
..
10.
Ninathibitisha kuwa taarifa zilizojazwa ni sahihi. Mwombaji huyu afikiriwe/asifikiriwe* kuwa Karani wa Sensa (kama asifikiriwe, taja sababu)
..
.
Jina la Mkuu wa Sehemu ya Kazi
.
Cheo
Sahihi na Muhuri
....
SEHEMU YA IIB:UTHIBITISHO KWA WASIO NA AJIRA(Ijazwe na Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa)
11.
Ninathibitisha kuwa mtajwa hapo juu ni mkazi wa Kijiji/Mtaa*
.
Kata ya
....
.
12.
Ninathibitisha kuwa taarifa zilizojazwa ni sahihi. Mwombaji huyu afikiriwe/asifikiriwe* kuwa Karani wa Sensa (kama asifikiriwe, taja sababu)
..
..
.
Jina la Afisa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa*
...
..
.
Sahihi na Muhuri
..
Tarehe
..
[SUP]
*[/SUP]
Futa lisilohusika