Dr naytham
New Member
- Aug 17, 2015
- 1
- 0
SHUKRANI NI MBEGU YA FURAHA
Tunaishi kwenye dunia yenye wingi wa vitu vizuri ambapo kwa wingi huo hutufanya tuendelee kutamani zaidi na zaidi kitu ambacho ni rahisi kusahau vile tunavyomiliki tayari.
Kwa kusahau huko hutufanya tuwe wengi wa watu wenye furaha fake,furaha ya mdomoni na sio moyoni.
Siri ya furaha ya kweli mara nyingi haipo katika kupata zaidi, bali katika kuthamini kile tulicho nacho na kushukuru.
Sayansi ya Shukrani
Wanasaikolojia na watafiti wamechunguza kwa muda mrefu athari za shukrani kwenye afya ya akili na furaha. Tafiti zinaonyesha kuwa na tabia ya kushukuru mara Kwa mara huboresha ustawi wa kihisia, hupunguza msongo wa mawazo, na kuimarisha mahusiano.
Shukrani hubadilisha jinsi ubongo unavyofanya kazi, ikiuandaa kupokea hisia chanya zaidi na kupunguza mtazamo hasi. Kwa hivyo, shukrani ni chombo kilichothibitishwa kuboresha ubora wa maisha yetu.
Ambapo kwa kushukuru mara nyingi
Watu hufaidika kama ifuatavyo
1.Shukrani hubadilisha Mtazamo: Kutoka Upungufu Hadi Utele
Mtazamo wa ukosefu kuzingatia kila wakati kile tunachokosa hutuweka kwenye mzunguko wa kutoridhika na kutokua na furaha halisi.
Kwa kukosa furaha tunajikuta kuwa tunajilinganisha na wengine, tunakimbiza malengo yasiyofikiwa, na tunajikuta tukiishi bila kuridhika na kuonea wivu wengine.
hivyo Kwa kushukuru tunabadilisha mtazamo wa namna tunatazama maisha yetu na wengine.
Shukrani huvunja mzunguko huu kwa kubadilisha mtazamo wetu kutoka ukosefu hadi utele.
Mfano;
Badala ya kuonea wivu mafanikio ya wengine ukianza kushukuru ubongo utakuelekeza kusherehekea hatua zako za mafanikio, hata kama ni ndogo.
Hutakua na wivu na wengine tena na utajenga muda mzuri na nafsi yako na utaridhika
Kwasababu miongoni mwa dalili za mtu asiyeridhika na maisha yake na kukosa furaha ni pamoja na kushughulika na kutazama mambo ya wengine zaidi.
Kwa kubadilisha mtazamo wetu, tunagundua kuwa tayari tunacho cha kutosha, na ufahamu huu huzaa furaha.
Njia zifuatazo zitakusaidia kuwa na tabia ya kushukuru na kufurahia maisha yako.
Kama ilivyo tabia nyingine, shukrani inahitaji mazoezi.
Hapa kuna njia rahisi za kukufanya kuwa mtu wa shukrani Kila siku katika maisha yako na hivyo kuwa mtu mwenye furaha.
1. Andika Shukrani Zako:
Kuwa na daftari la shukrani ili Kila siku uwe unaandika vitu vitatu unavyoshukuru. Zoezi hili linafundisha akili yako kuona mambo chanya na utajikuta mara nyingi una furaha itokayo moyoni.
2. Toa Shukrani kwa Wengine:
Kuwa na utaratibu waambie watu katika maisha yako jinsi wanavyokufaa
Neno la upendo au asante ya dhati huimarisha mahusiano na kuinua mioyo.
3. Fanya Mazoezi ya Kujitafakari:
Tenga muda wako Kila siku wa Kujitafakari na kujithamini.
Uwe unajipa kipaumbele kujijua jinsi ulivyo na Yale unayotaka maishani.
4. Shukuru Changamoto zako ili kuwa na Mtazamo Chanya:
Hata katika nyakati ngumu,fahamu kuwa Kuna baraka zilizojificha.
Shukrani haimaanishi kupunguza changamoto bali kutambua mazuri yaliyomo ndani yake.
Tunashukuru Kwa kuumwa ili tuthamini nafasi ya uzima
Tunashukuru Kwa kukosa chakula ili tujue uchungu wa njaa
Tunashukuru Kwa Kila kitu sababu ndani yake zipo Baraka.
Fikiria maisha yako kama bustani. Kila shukrani unayotoa ni mbegu unayopanda. Kwa uangalizi na utunzaji, mbegu hizi hukua na kuwa maua yenye rangi ya furaha, na kuridhika.
Unavyopanda shukrani zaidi, ndivyo bustani inavyozidi kutoa maua ya furaha.
Furaha si kuwa na kila kitu unachotamani; ni kuthamini kila kitu ulicho nacho. Kwa kuzingatia shukrani, si tu unabadilisha mtazamo wako, bali pia unakuza maisha ambayo furaha inachanua bila juhudi nguvu za nnje.
Leo tenga nafasi ya kushukuru kuhusu maisha yako Kwa mambo uliyotengeneza hapa duniani.
Kliniki ya Furaha
0746465095
#klinikiyafuraha
#pingaupweke
#ChaguaFuraha
#upwekeunaua
#mapenzi
#amaniyandani
#sautiyandani