Game Theory,
..Nafasi ya Waziri Mkuu ni moja ya vipengelea vya katiba mpya ambavyo viliwakosanisha Raila na Kibaki.
..Hata kwenye ile Constitutional Referendum Kibaki alikuwa akipinga nafasi ya Waziri Mkuu na Raila akiunga mkono.
..Kwa msingi huo nachelea kuamini kwamba idea ya PM imetokea Tanzania. Hata Uganda wana Waziri Mkuu. Mozambique wana Waziri Mkuu. Zanzibar wanaye Waziri Kiongozi/Waziri Mkuu. Kwanini Watanzania tunasisitiza idea hiyo imetokea kwetu tu, na siyo nchi nyingine yoyote?
..Hapa Tanzania tumekuwa na mjadala mkali kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu vs Makamu wa Raisi. Kuna wanaodai kwamba moja ya nafasi hizo ni redundant. Sijui kama mjadala kama huo hautatokea Kenya.
..Kwa upande mwingine inasemekana Kikwete alikwenda Nairobi na kumpa somo Mwai Kibaki kuhusu nafasi ya Waziri Mkuu.
..Kwanini Mwai Kibaki alishindwa, kwa mwezi mzima, kuelewa somo la Uwaziri toka kwa Ben Mkapa au hata Graca Machel, lakini kwa muda wa masaa kadhaa tu akaelewa somo hilo hilo toka kwa Jakaya Kikwete?
..Ndiyo maana kuna wanaodai kuna kitu kilichojificha kuhusu safari ya Kikwete kwenda Nairobi. Hali hiyo ndiyo inayowafanya watu waamini kwamba Kikwete alikuwa ametumwa na wakubwa kwenda kuwatisha na kuwalazimisha Mwai Kibaki na Raila Odinga kufikia makubaliano ya amani.
..Lakini hata kama hakuwa ametumwa na wakubwa, kabla Raisi Kikwete hajatua Nairobi,Raisi Museveni alikaririwa akisema kwamba usuluhishi utapatikana. Kikwete naye alikaririwa akitoa kauli kama ile ya Museveni.
..Je, haiwezekani kwamba Koffi Annan na timu yake walishafanya vitu vyao? Haiwezekani kwamba Kikwete alikuwa anakwenda kukamilisha kazi kama Mwenyekiti wa AU? Kumbuka kwamba mazungumzo haya yalianzishwa na John Kuffour wa Ghana kwa wadhifa wa Uenyekiti wa AU.
..Makubaliano ya amani ya Kenya yana vipengele vingi ikiwemo kuanzishwa kwa Tume za kuchunguza masuala ya Ukabila, Tume ya usuluhishi na Ukweli[truth & reconciliation], Uchunguzi wa uchaguzi na muundo wake, na marekebisho ya katiba. Haiyumkiniki Raisi Kikwete akae Nairobi kwa siku mbili na kukamilisha mambo yote hayo.
..NINAAMINI KUNA JITIHADA ZA MAKUSUDI KABISA ZA KUMSIFIA NA KUMKWEZA RAISI KIKWETE KWA KAZI AMBAYO HAKUIFANYA. WAKATI HUOHUO TUKIDHARAU JUHUDI NA KAZI ZA WASULUHISHI GRACA MACHEL,BEN MKAPA,OLUYEMI ADENIJE, CHINI YA UONGOZI WA KOFFI ANAN. HATA MAHASIMU WAWILI RAILA NA KIBAKI HAWAPEWI SIFA YOYOTE ILE KWA UJASIRI NA MATURITY WALIOONYESHA KUFIKIA MAKUBALIANO HAYA.