Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Kwa niaba ya Waandaaji wa wiki ya Maandamano ya Amani (awamu ya kwanza) na kwa niaba ya Wapenda haki wote duniani, nachukua Fursa hii kuwashukuru watu wote kutoka pande waliowezesha Maandamano hayo kufanikiwa na kutikisa kwa kishindo, ambapo imedhihirika sasa kwamba yameacha gumzo Duniani kote.
Shukrani ziwafikie wote kabisa waliosambaza taarifa za Maandamano hayo kote duniani, tunaishukuru sana JF kwa kuruhusu taarifa za Maandanano hayo kuwemo humu 24/7 bila kikwazo chochote, pamoja na vurugu za wahafidhina za kuchomekea lugha chafu ili kutukatisha tamaa, kwa kweli tutakuwa wachoyo wa fadhila ikiwa tutashindwa kumshukuru Waziri wa Habari Mh Nape Nnauye, ambaye alitumia muda wake vizuri kusambaza taarifa za Maandamano hayo ndani ya Bunge la Tanzania, tena aliyasambaza kwa weledi na kwa usahihi kabisa.
Bali hatuna cha kuwalipa wale waliowezesha Maandamano hayo kwa hali na mali, kwa dua na maombi, kwa pesa na michango yao yote waliojitolea, Tunamuomba Mwenyezi Mungu awarudishie ukarimu wao mara nyingi zaidi ya walichotoa, Kazi waliyoichangia ni kazi ya Mungu mwenyewe kabisa na ndio maana mnaona Kishindo cha Tanganyika
Mungu ibariki Chadema, Mungu Ibariki Tanganyika